Saturday, January 28, 2017

MUZIKI WA KIZAZI KIPYA NA DOMO LANGU ZITO.

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO



MUZIKI wa kizazi kipya umepita katika kipindi kigumu sana hadi kufikia kukubalika kwa jamii,hasa kwakuwa kulikuwa na muziki tangulizi ambao
ulikuwa umezoeleka katika masikio ya Watanzania.

 Haikuwa rahisi kumudu kuupiku muziki wenye miondoko ya Rhumba,Reggae na hata muziki wa Taarabu.Na umeendelea kuwa na changamoto ya kukubalika katika jamii kutokana na tunzi zake zilizo nyingi kuwa na ujumbe mwepesi,anaandika Jackson Bahemu.

Pamoja na changamoto hiyo,vijana walioasisi muziki huo nchini wakiwemo akina Waheshimiwa amabao hivi sasa ni wawakilishi wa wananchi katika majimbo ya Mikumi,Joseph Haule “Profesa Jay”na Joseph Mbilinyi “Sugu” wa Jimbo la Mbeya Mjini,wakishirikiana na akina Kasimu Kiroboto “Juma Nature”.

Pia Balozi,Solo Thang,Zay B,Sister P,Inspector Harun,Soggy Dog Hunter na wengine kibao,walikabiliana na changamoto ya kutokubalika kwa kuhakikisha wanaandaa mashairi mazuri,na kutoa muongozo wa tunzi zenye maadili katika Nyanja za maisha,hususani mapenzi.

Kadri siku zinavyosonga mbele ndivyo muziki huo unazidi kukubalika na kuibuka kwa Wasanii ambao wamendeleza libeneke kwa kuandika na kuiba mashairi mazuri yenye ujumbe.

DOMO LANGU ZITO  Ni moja ya nyimbo za Kitanzania zenye ujumbe mpana na wa kina zaidi katika lugha ya Kiswahili chenye mafumbo.Msanii katika wimbo huo,Timbulo amejaribu kufikisha ujumbe kwa njia ya kuimba kwa mafumbo,na kwa  kiasi kidogo kwa uwazi.

Timbulo ambaye kwa taaluma,ni Mwalimu ambaye alisomea na kumudu kuitumikia kwa muda kabla ya kuamua kupumzika,kwa ajili ya muziki,ambao nao umeonesha kutomkimbia hasa kutokana na utunzi wake katika wimbo huo,ambao umedhihhirisha kuiva katika taaluma ya ualimu kwa jinsi alivyocheza na Lugha hii adhimu.

  Domo ni neno la Lugha ya Kiswahili lenye maana ya mdomo,  akiwa na maana mdomo wake mzito(Domo langu zito) ni pale unaposhindwa kusema jambo likukelalo ama ulipendalo lakini woga unakujaa zaidi.

"Nambie nijue naona kama nakulazimisha nawe ushampenda mwenginee..nijue nisikusumbue moyo wangu hauitaji kugeuzwa kama chapati.";

Mistari hiyo,anaonesha ni kiasi gani anapenda,lakini  anahisi kama vile mwenzie anamsumbua ama hamsumbui yawezekana anamfikiri au ana mambo mengine lakini anajipa majibu yakuwa yawezekana kuwa kesha mpenda mwingine au yuko katika mapenzi mengine na mtu mwingine.

  Kwakuwa ni mzito wa kutoa yaliyoko moyoni mwake ama Yale atakayo apate, kunamfanya ajenge hisia tofauti juu yake na kumfanya awe mwoga zaidi kutoa yaliyoko moyoni kwake kwa kuhofia kutendewa mambo yasiofaa,ambayo pengine  yatautesa moyo wake na kuumiza kwa fikra.
 
   "Moyo wangu hauitaji kugeuzwa kama chapati" ni maneno ambayo ni ya Kiswahili yakiwa katika mafumbo kidogo ,moyo kugeuzwa kama chapati, juu chini ,ndani nje,kupakwa mafuta ili kulainika,ama vinginevyo.Hii inaonesha ni jinsi gani katika mapenzi watu hususani vijana hutendeana kama upikaji wa chapati na kuumizana kama ambavyo Timbulo analalamika.

  Unapendwa leo kesho umeachika unakuwa na huyu kesho yule anakupa mapenzi mazito lakini yasodumu na hukauka muda mchache so ametoa somo zuri kuacha kugeuzana kama chapati ipikwapo na kuonesha upendo uliojaa na usiofichika ama uongo.

" Sidhani kama na kosa moyo wangu wanisumbua domo langu zito kumwambia kweli nashindwa"

  Kupenda ni haki na haimaanishi kuwa ni kosa pale atakapo amua kutompenda au kumpenda yule amvutiae japo mdomo wake mzito kusema kile atakacho ama apendacho kunena kwani utakuwa niukweli kutoka moyoni ama kinywanj mwake.

   Usishindwe kufikisha kile utakacho kusema ikiwa umemwona mlengwa ama muhusika mwenyewe kwani itakuweka huru na hutaweza kulifikiri sana na ukifikiri sana utapata majibu ambayo so sahihi juu ya kile utakacho,anaendelea.
 
"Nashangaa msichana mzuri kama wewe Dada ukaukabidhi moyo  takisi  driver ...asubuhi yeanenda...amekuliza jioni sipati kusema "

  Msanii huyu kajaribu kutumia neno taksi dreva ilikufikisha ujumbe lakini wenye fumbo gumu kidogo.Kwani nani asiyemjua taksi dreva na majukumu yake?Hakika najua mnamjua taksi driva hubeba abilia mpaka mwisho wa safari ama katikati ya safari na kuwashusha ama hubeba wengine .

    Unapomkabidhi mwanaume penzi ama nafsi ya hisia zako za kimapenzi bila umakini wa kutosha utakuta ukimkabidhi mchezeaji na mbebaji wa abiria wengi jioni na asubuhi anakuacha ukilia na machungu ya mapenzi bila kujua yeye ni taksi driver tu.

    Kumbe hata kwako alikuwa akipita tu na alikupa lifti ya wewe kuhisi umefika kumbe yeye ni kawaida kwake kuwapa na kuwaacha asubuhi na jioni ni kilio,msanii kaingia ndani na kuonesha ni  jinsi gani anavohisi pindi anapowaona
 
" nalia naumia kila Siku nikiwaona chozi langu la huruma kweli acha lidondoke ......?sijui ni mchane ila asinitukane..?Akinitema itakuwa soo"

 Huo ni ubeti aliouandaa kwa mtindo wa kusaili na katika Lugha ya Kiswahili cha kisasa zaidi,kuna neno la ujana zaidi wa mitaani; (ni mchane) ni neno la kiswahili lakini lipo katika athari za lugha za mitaani ama vijiweni ilipaswa kuwa Nimwambie ama vingine iwavyo katika lugha fasaha au ufupisho katika ushairi na mafumbo pia.

   Na msanii kuonesha hisia zake kwa kusema yaliyoko moyoni kwake kulia na kuumia kwani angelia bila kuumia ni sawa anaecheka mpaka kulia amakufurahi lakini kuumia ni maumivu ya  upendo hasa pale anapowaona na chozi la huruma linamdondoka kwa uthibitisho.

   Inamaana unampenda mtu lakini yeye hajitambui na anajikuta akiingia katika mapenzi na mtu mwingine asiye jua thamani ya kupenda ama maumivu ya kutendwa japo yupo tuu na wewe kwa yule mwenye uchungu na kupenda ama mapenzi ya kweli anaumia sana na kwa huruma zaidi hudondosha machozi kweni hamtadumu katika mahusiano yenu ama mapenzi yenu.
 
   Na jambo la mwisho katika ubeti huu msanii katumii swainglish yaani neno la Kiingeleza kuwa na maana ya ndani katika Kiswahili.

Neno SOO ameitumia akimaanisha(mbaya) iliyokithiri na kama vile hakuachia hapo akaongeza na lugha za kimtaani/vijiweni kunitema,ni tendo la kutoa mate mdomoni kwenda chini, sasa hapa msanii alimaanisha nini??

  " akinitema itakuwa soo" kutema limetumika mbadala wa kuniacha,kunikataa,kunitupa na vile iwavyo kwa kiswahili fasaha itakuwa na maana ya ( akinikataa itakuwa mbaya /hatari) na vingine pia  ni moja ya utunzi wa shahiri nyingi na beti nyingi ili kufikisha ujumbe kwa jamii husika,anamalizia kwa shairi hili.

" angejua angenipa nimpe leo niwenyuu ni bahati kwa wake upendo......upendo wangu ni kama ziwa.....Penzi lako tamu kama asali zaidi ya vanilla ..yeerereryerere.. nalia naumia kila siku nikiwaona chozi langu la huruma......."

  Ukitizama jinsi anavyoeleza msanii huyu wa kizazi kipya utagundua nini kamaanisha na nini kafikiria katika nyimbo yake hii,ambayo hapana shaka ni kumbembeleza na kumsihii mwanamke anaempenda juu ya kile alichonacho yeye na kumsifu ili ampate ili kukidhi hitaji lake.
 
   Anajua hajui afanyalo pia aendako kama angejua angempa leo na kumuonesha yeye anaupendo kiasi gani ama mapenzi yake yalivyo kama ziwa sasa hapa kaingia katika kina cha kuonesha upendo wake haupimiki.
 
    Na kama haitoshi analisifia penzi la yule amtakae kwa kuonesha penzi lake ni tamu kama asali zaidi ya vanilla ilihali hajapata kulionja so hapa ukiona kina kunanamna anajarbu kuvutisha hisia za kile aonacho na atafutacho kwa kukipa sifa zaidi wakati hajapta penzi la huyo amtakaye.

  Kiujumla kajitahidi sana msanii kufikisha ujumbe aliokusudia na dhamira yake kuu imefika kwa wahusika ama hadhira Mapenzi na wakati unataka upendo ama mapenzi unakuwa mzito mdomo wake kuongea inakupa wakati mgumu kwa maumivu.
 
    Pia katika kuwasilisha sanaa lazima kuzingatia matumizi ya lugha na mahali husika,pia kutokuchanganya maneno ya lugha flani na flani kama Niwe nyuu na soo na ili kuifanya kazi ya fasihi kwa weledi na uimara mkubwa ni lazima tutumie lugha fasaha maneno kama kunitema na nimchane ni maneno ya mitaani.

      Ambapo hata kusudi la wimbo ama mtunzi halita wafikia walaji au wasikilizaji na kushindwa kuujua umuhimu na umaudhui  ya huo wimbo katika jamii nzima. Hongera sana Timbulo kwa utunzi mzuri na uliosheheni ujumbe tosha katika mapenzi.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI