WAKATI
Januari 15,mwaka huu,Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) ikitangaza wanafunzi
67,547 wa darasa la Nne nchini,kurudia darasa hilo,kutokana na mtihani uliopita
kupata alama zenye ufaulu usioridhisha.
Huku
wanafunzi waliofanya mitihani hiyo,wakishindwa zaidi katika masomo ya Hisabati
na Kiingereza,Mjukuu wa aliyekuwa Waziri katika wizara kadhaa za Serikali ya
Awamu ya Tatu na ile ya
Awamu ya Nne;Professa Juma Kapuya,ametunga kitabu cha
ziada kwa somo la Kiingereza.
Mjukuu
huyo wa Professa Kapuya;Farid Hamamad,ametunga kitabu hicho kujaribu kupunguza
changamoto inayoikabili Serikali ya uwepo wa vitabu vya ziada katika shule za
msingi nchini,hususani katika somo la kiingereza ili kuleta chachu ya wanafunzi
kufanya vyema katika mitihani yao ya mwisho.
Hamamad
anasema anatambua umuhimu wa sekta ya elimu kwa maslahi ya Taifa,pia changamoto
iliyopo ya uhaba wa vitabu vya ziada katika shule za msingi ambavyo uwepo wake
kwa wingi huku vikitumika ipasavyo ni siri ya ufaulu mzuri wa wanafunzi.
Anasema
maendeleo ya kiuchumi ya Taifa lolote duniani ni sekta ya elimu,na kwakuwa kiu
yake kubwa kuona Tanzania inamiliki uchumi imara,ambao chachu yake itakuwa ni
wasomi ndio maana kapata hamasa ya kuandika kitabu cha somo hilo ambalo mara
nyingi huwa kikwazo cha ufaulu mzuri kwa wanafunzi.
“Tunaupungufu
wa vitabu vya ziada nchini,hasa katika shule za msingi,hususani kwa somo la
Kiingereza,ndio maana hata ufaulu wake kwa watoto waliofanya mtihani wa darasa
la nne,mwaka jana ni asilimia 12.51,nimeumia sana kwa ufaulu huo kwa Taifa
ambalo lina mkakati wa kukuza uchumi wake kwa kuanzisha viwanda,ndio maana
nimeona nisaidie kwenye hilo,”alisema Hamamad.
Anabainisha
kwamba kitabu hicho cha ziada,kina maswali na majibu kwa wanafunzi,ambayo ni
mazoezi yatakayokuwa msaada kwao wa kufanya vyema katika mitihani ya Kiingereza
kwa darasa la nne na ile ya kuhitimu elimu ya msingi,pindi wakikitumia vyema
kwa kufanya mazoezi ya kutosha.
Katika
mitihani ya darasa la nne iliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana,wanafunzi
1,054,191 walisajiliwa,lakini waliofanya mtihani walikuwa 1,017,776 na miongoni
mwao asilimia 6.64 wakipata alama za daraja E,lenye ufaulu usiorodhisha na
hivyo kulazimika kurudishwa mwaka huu kusoma darasa la nne tena.
Wanafunzi
walifanya vyema katika somo la Stadi za Kazi,Haiba na Michezo kwa kufaulu kwa
asilimia 94.67 na kuanguka zaidi katika somo la Kiingereza.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI
1 comments:
Write commentsAnalosema Hamamad ni la kweli kabisa, tunachangamoto nyingi sana katika elimu Tanzania, Nakupa pongezi kwa kujitokeza kusaidia wanafunzi mashuleni, waweze kuelewa na kufahamu lunga ambayo inatumika ulimwengu mzima katika kila sekta ya Maisha, hususan Uchumi. Kila mwenye kipaji chake akikutumia kwa lengo la kukuza elimu, na kusaidia watanzania wenzake, Tanzania itakua Nchi Bora na Imara katika bara la Africa na Ulimwengu kiujumla
Reply