KATIKA
kukomesha uharifu na kuhakikisha sherehe za Krisimasi na Mwaka Mpya
zinasherehekewa kwa amani,Jeshi la polisi mkoani Shinyanga limeanzisha
opresheni maalumu kwa kutumia vitabu vya
kumbukumbu za zamani kusaka majambazi sugu na kufanikiwa kukamata wanane.
Mkakati
wa Opresheni hiyo umeanzishwa baada ya vitendo vya kiharifu wa kutumia silaha
kuanza kujitokeza kwa kasi tangu mwezi Oktoba mwaka huu,na kuanza kuwatia hofu
wakazi wa mkoa wa Shinyanga.
Akiongea
na Waandishi wa habari mjini Kahama,Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, Murilo
Jumanne,alisema katika uchunguzi wa
awali wa Jeshi hilo ulibaini matukio hayo kuibuka baada ya waharifu waliokuwa
wamefungwa na baadae kuachiwa kwa kukata rufaa na wengine kumaliza adhabu zao.
Kamanda
Jumanne alifafanua kuwa kwa mujibu wa sheria za nchi,kukata rufaa kwa mhalifu
ni haki yake,lakini kitendo hicho hakiwakatishi tamaa bali watawajibika kwa
kufuata kanuni za jeshi la Polisi kuzuia uhalifu kwa kuwasaka wote ambao vitabu
vyao vya kumbukumbu vinaonesha ni waharifu na majambazi sugu wa kutumia silaha.
Alisema
tangu mwezi Oktoba mwaka huu,uharifu ulianza kujitokeza kwa kasi katika wilaya
za Kahama,Shinyanga na Kishapu,hivyo kurejea katika vitabu vyao vya kumbukumbu
za waharifu kubaini wapo wapi ndipo walipobaini wengi
wameachiwa kwa rufaa na wengine kumaliza vifungo vyao.
“Tulipobaini
kuwepo kwa waharifu nje,tulijiuliza kwanini vitendo hivyo vianze wakati watu
hao wakiwa uraiani?” Alihoji Kamanda Jumanne.
Kufuatia
hali hiyo upelelezi ulianza kuwafuatilia na kubaini kundi moja la
majambazi wanane wakiwemo wanawake wanne ambao wamekamatwa wakiwa na bunduki 2
shoti gun ambazo zimekatwa mtutu na kuonekana kama bastola.
Pia
kamanda Jumanne alisema watuhumiwa hao walikutwa na pikipiki 2 zenye namba moja
MC476 BHA ambazo zimedaiwa kutumiwa kuwapeleka kwenye matukio ya
uharifu na kuongeza kuwa katika upelelezi huo mtuhumiwa mmoja Amosi James au
maarufu kwa jina la George alifariki baada ya kupigwa risasi na polisi.
Katika
tukio hilo mtuhumiwa huyo alikamatwa na bunduki 3 moja SMG na mbili shoti gun
na risasi 38, risasi 30 zilikuwa kwenye magazine na aliwashawishi polisi ana
bunduki nyingine kwa mganga wa jadi maeneo ya Busoka na baada ya kufika huko
aliruka kwenye gari na kuanza kukimbia hali iliyofanya kupigwa risasi na
baadaye kufariki wakati anapelekwa hospitalini.
Kamanda
Jumanne,alisema baada ya kufanya
upelelezi juu ya mtuhumiwa huyo na kundi lake walibainika kufanya uharifu
katika maeneo mbalimbali ya kanda ya ziwa ikiwemo Kahama, Shinyanga, Bukombe,
Mbogwe na Geita na alikuwa amefungwa gerezani na akatoka kwa rufaa.