Wednesday, November 9, 2016

WANAFUNZI 21 WA SEKONDARI WAKATISHWA MASOMO KWA MIMBA KAHAMA.

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO



IMEFAHAMIKA vitendo vya unyanyasaji wa kingono kwa watoto wa kike wanaosoma Shule za Sekondari wilayani Kahama vimekithiri na kusababisha wanafunzi 21 wa Shule za Sekondari za Kata katika
Halmashauri ya Mji wa Kahama,kukatisha masomo kutokana na kupata ujauzito.

Katika utafiti uliofanywana Shirika lisilo la Kiserikali la SHDEPHA+ la wilayani Kahama,limebainisha takwimu za wasichana hao kukatisha masomo kwa kupewa ujauzito ni kuanzia mwezi  Januari hadi kuishia mwezi Septemba mwaka huu.

MKURUGENZI Miradi SHDEPHA+,Venance Mzuka akiongea.
Akiongea na waandishi wa Habari  Mkurugenzi wa Miradi wa SHDEPHA+, tawi la Kahama linalojihusisha na masuala ya ukatili wa kijinsia,Venance Mzuka,alisema  wanafunzi hao wamepatiwa mimba hizo kwa kubakwa na wengine kurubuniwa na vitu vidogovidogo.

“…walichofanyiwa ni unyanyasaji wa kijinsia,na vitendo hivyo vikifumbiwa macho ni hatari kweli kwa taifa kutokana na wasichana hao kukatishwa masomo yao,”alisema Mzuka.

WANAHABARI wakisikiliza kwa makini
Alizitaja shule ambazo zimeripotiwa kwa kipindi hicho wanafunzi wake kupatikana na ujauzito ni kutoka shule za Abdurahim kata ya Busoka, Seeke, Kishimba, Nyasubi, Nyihogo, Mwendakulima, Bukamba huku Nyashimbi ikiwa kinara wa mimba hizo baada ya kuwa na wanafunzi saba waliokatisha masomo kwa ujauzito.

MZUKA akikisisitiza jambo kwa Wanahabari
Hata hivyo alisema Shirika lake limeweka mkakati wa kuwajenga kisaikolojia   waliokumbwa na kadhia hiyo na kukatishwa masomo, ili warejee katika masomo yao,kutokana na kutambua matendo hayo ya ubakaji ama kurubuniwa na kujikuta wakifanya ngono,kitendo kinachoshusha uwezo wao darasani.

WAANDISHI wa Habari;Shija Felician na Pili Jitoba.
Kwa upande wake,Msimamizi wa Kesi za Unyanyasaji wa Kijinsia katika Shirika hilo,Kazungu Barnabas, alisema matendo hayo kwa mimba za wanafunzi yanakithiri kutokana na uchukuaji wa hatua za kisheria kwa wanaume wanaowapa mimba wanafunzi,kuwa mgumu.

“….wabakaji hao hufanya maelewano,kisha kulipa fedha au mifugo,na familia wa binti na kesi hizo kuzimalizia majumbani,huku wazazi ama walezi wakiandaa hadaa ya kutotiwa hatiani,”alisema Barnabas.

MZUKA akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari
Nae Meneja Mradi wa Sauti kutoka  Shdepha+ ,Shekha Nassoro, alisema kukithiri wa vitendo hivyo kunatokana na watoto hao kutokuwa na uelewa sambamba na kufahamu pa kukimbilia  wanapofanyiwa ukatiri huo, hali  inayochangia kufanyiwa vitendo vya ukatiri bila kujua kama wamefanyiwa vitendo vibaya.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Kahama,Anderson Msumba,alikiri kuripotiwa kwa baadhi ya wanafunzi kukatiza masomo kutokana na mimba,kiasi cha kuamua kukabiliana na hali hiyo kwa kuweka utaratibu wa kupima mimba kwa wanafunzi wa kike kila baada ya miezi mitatu.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI