Thursday, October 20, 2016

WANAUME WADAIWA KUFANYIWA VITENDO VYA UKATILI NA WAKE ZAO

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO



PAMOJA na vitendo vya Ukatili wa kijinsia kukithiri huku ikidaiwa wanaume ndio vinara wa matendo hayo,lakini imebainika Wilayani Kahama   kuna wanaume wanaofanyiwa ukatili wa kijinsia na wake zao, lakini wanaogopa
kuripoti Polisi kwa kuhofia kujidhalilika.

Wanashindwa kufika katika kituo cha polisi mjini Kahama kuripoti vitendo wanavyofanyiwa na wake zao kwa hofu ya kujidhalilika kwa jamii ikiwa ni pamoja na kuogopa kuachika kwa wake zao,gazeti hili tando la Lifali,linaeleza.

Jeshi la Polisi kitengo cha dawati la jinsia na watoto,wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga, lilinabainisha kwamba kuna baadhi ya  Wanaume  ni waathirika, lakini hawaripoti vitendo wanavyofanyiwa na wake zao kwa hofu ya kujidhalilisha.
 
Mkuu wa kitengo cha dawati la jinsia Wilayani hapa,Koplo Ninaely Kisagase,aliyasema hayo wakati alipotembelewa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhil Nkurlu,katika banda lake la maonyesho siku ya maadhimisho ya nenda kwa usalama barabarani. 

Kisagase akiwa katika viwanja vya CDT mjini Kahama, ambako  maadhimisho hao ya nenda kwa usalama barabarani yalifanyika Kimkoa,alimweleza mkuu huyo wa Wilaya kuwa wapo wanaume wanaofanyiwa vitendo vya kikatili na wanawake zao lakini wanashindwa kuwaripoti polisi kwa kulinda heshima na ndoa zao.

Alimuhakikishia Mkuu wa wilaya kuwa Jeshi la Polisi, linafanya kazi kwa ufanisi na usiri mkubwa,hivyo kuwaomba wanaume watoe taarifa katika kitengo cha dawati la Jinsia na watoto,ambapo wataketi pamoja na kuwashauri,katu hawawezi kuharibu ndoa. 

“Na kama mwanaume atashindwa kumripoti Polisi mke wake anaweza kuathirika kisaikolojia jambo ambalo ni hatari sana kwa familia na jamii inayomzunguka na vitendo hivyo kama vitagundulika kufanywa kwa makusudi tutafungua jalada na kuwapeleka Mahakamani kwa sharia zaidi.
.”Aliongeza Kisagase.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kahama Fadhil Nkurlu alilitaka jeshi la polisi kuhakikisha linazidi kuimarisha hali ya usalama ndani na nje ya Wilaya ya Kahama na Mkoa wa Shinyanga kwa ujumla na kuwataka kutomfumbia macho raia yoyote anayevunja sheria za nchi zikiwamo za barabarani.

Pia alilitaka jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani kutochukua rushwa kwa wavunja sharia barabarani hali ambayo itasaidia kupunguza ajari barabarani pamoja na kuondokana kwa mazoeya mabaya baina ya askari na madereva

Hata hivyo mkuu huyo wa Wilaya alilitaka jeshi la polisi kudhibiti vitendo viovu vya madawa ya kulevya,Viroba,mirungi na bangi na kuongeza kuwa madereva wanapotumia virevi hivyo husababisha wajione wako sahihi barabarani japokuwa wamekiuka sharia hizo.

Anasema;“Ajari nyingi zinazotokea barabarani zinasababishwa na jeshi la polisi kwa kitendo cha kuchukua rushwa kwa waliovunja sheria za usalama barabarani."

"...acheni kuchukua hizo rushwa hali hiyo itasaidia kupunguza mazoea mabaya baina yenu Askari na watumia barabara,na ikumbukwe sheria ya jeshi la polisi inakataza polisi kujihusisha na kupokea rushwa ama kutoa rushwa”,alisema Nkurlu.







KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI