Friday, October 21, 2016

TAKUKURU KAHAMA YALIA KUSHINDWA KESI

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO



TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa( TAKUKURU) Mkoa  malumu wa Kahama,unalia kushindwa kesi kunatokana na jamii kuwa na uelewa mdogo juu ya kutoa ushahidi Mahakamani.

Wananchi wamekuwa na tabia ya usaliti kwa TAKUKURU, katika suala la kujitoa kuwasilisha ushahidi,hivyo kusababisha kushindwa
kwa kesi nyingi zinaikabili Taasisi hiyo,anaandika Shaban Njia. 

Imedaiwa Wananchi wamekuwa wakitoa ushirikiano hasa pale wanapokuwa wakitoa maelezo ya awali,inapofika wakati wa kufikishana mahakamani wamekuwa wamekuwa wakikanusha maelzo yao huku wengine wakisema kuwa wameandika maelezo kwa kitishiwa aidha kwa silaha au vitu vingine. 

 Akizungumza  katika kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani katika halmashauri ya mji wilayani Kahama,Mkuu wa Takukuru Mkoa maalumu wa Kahama,Chrisantus Ndibaiukao alisema kuwa kesi inapofika mahakani mtoa ushahidi amekuwa akikanusha ushahidi ambao alitoa nakuongeza kuwa ushahidi huo ameutoa kwa kulazimishwa. 

"Tumekuwa tushindwa kesi nyingi kutokana na ushirikiano mdogo wawananchi kutoa ushahidi hasa pale kesi zinapokuwa zimepelekwa mahakamani na wamekuwa wakikataa kile ambayo kimeandikwa na wakisema kuwa wamelazimishwa kuandika ushahidi huo" alisema. 
Aidha Ndibaiukao alitaja kesi ambazo zimeshafikishwa mahakamani ni tisa huku kesi tatu zilitolewa maamuzi na walengwa walichukuliwa hatua za kisheria, nakuongeza kuwa kesi nyingine tatu zilishindikana kutolewa ufafanuzi kutokana na kutotolewa ushahidi vema toka kwa wananchi. 

Hata hivyo aliwataka wananchi wanatoa taarifa katika ofisi za takukuru juu ya vitendo viovu vya rushwa kutoa ushirikiano hasa pale kesi inapofika mahakamani nakuongeza kuwa hali hiyo itapelekea kushinda kwa kesi na sio kushindwa na kukatia rufaa.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI