Friday, October 14, 2016

WAJENGA SHULE KUNUSURU WATOTO KULIWA NA FISI

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO



TISHIO la watoto kuliwa na fisi wanapokwenda shuleni katika kijiji cha Busulwangiri,Kata ya Bulyanhulu katika Halmashauri ya Msalala,wilaya ya Kahama,Mkoani Shinyanga,limesababisha kufanyika hamasa ya kujenga shule,kuwanusuru vijana wao kukumbwa na kdhia hiyo.

Hamasa hiyo imefanywa na Wananchi wa kitongoji cha Kolandoto,kijijini Busulwangiri  katika Kata ya Bulyanhulu,ambao miongoni mwao,watoto wao waliishaliwa na fisi,wakati wakienda shule iliyo mbali na eneo wanaloishi,anaandika Paschal Malulu.

Maamuzi ya wananchi wa kitongoji hicho,kujenga shule kwa kujitolea ili kunusuru watoto wao kuliwa na fisi,kutokana na umbali uliopo kwenda kwenye shuleni, ambayo ili kuifikia,kuna msitu mkubwa unaokaliwa na wanyama hao hatari kwa maisha ya binadamu.

Mwenyekiti wa kijiji cha Busulwangiri,Joram Kudisa,alisema kitongoji hicho cha Kolandoto,kiko umbali wa kilometa 12 kufika katika eneo la shule ya msingi Busulwangiri,hivyo kusababisha kuwepo kwa matukio ya watoto kuliwa na fisi.

Baada ya kukithiri kwa matukio hayo ya watoto kuliwa na fisi,wazazi katika Kata hiyo walianzisha utamaduni uliowalazimisha kila siku asubuhi kuwavusha watoto wao wadogo katika eneo hilo la msitu,ili kuwalinda wasiliwe na mnyama huyo.

Mwenyekiti huyo alieleza hayo mbele ya ujumbe kutoka mradi wa kuboresha elimu Tanzania Equip ambao ulitembelea kijiji hicho kuona juhudi zinazofanywa na wananchi hao kuboresha elimu na kuongeza tija kwa watoto wadogo kwenda shule baada ya kuanza ujenzi wa shule katika eneo hilo

Alisema kwa kuanza wamejenga  vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja ambayo itatumika kwa masomo ya awali na darasa la kwanza na la pili,kwa ajili ya watoto wenye umri wa miaka minne hadi saba,ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa wakisoma kwenye mazingira magumu na hatarishi.

Anasema;“…hasa wakati wakienda shule ambapo mara nyingi hufukuzwa na fisi kwa lengo la kuliwa tofauti na wale watoto wakubwa ambao wanauwezo wa kukimbia”.

  Kudisa alibainisha kwamba kwa kuanza shule hiyo itakuwa na watoto wenye umri huo  85,ambapo tayari kaya 96 kutoka kitongoji hicho, zimechangia ujenzi huo.

Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohamed Kahundi.alisema serikali itafanya jitihada za kuhakikisha ujenzi wa shule hiyo unakamilika mapema na kuanza kazi,huku akichangia Shilingi Laki Moja,kuwaunga mkono wanakijiji hao ambao tayari walikwisha kuchanga Shilingi  Laki Tisa.
Hata hivyo Kahundi aliwakumbusha kwamba pamoja na juhudi hizo,ni budi shule hiyo iwe na vyoo,pasipo kujali idadi ya vyumba va madarasa,kwa kuhadharisha kuwa  hata kama shule ingekuwa na vyumba 10 bila kuwa na choo haiwezi kufunguliwa.

Alisisitiza serikali haitakuwa taari kuifungua shule ikiwa na mazingira ya hatari kama hayo, na kuongeza kuwa shule haiwezi kuanza bila kuwa na choo,na kutaka suala hilo lipewe kipaumbele,ndipo kwa kutumia mamlaka yake ya  afisa elimu mkoa atahakikisha analeta walimu mapema iwezekanavyo, ili iweze kuanza mapema.

Kwa pande wake mwakilishi wa Equip Tanzania Victoria Mushi alisema mradi huo umekuwa ukitoa ushirikiano mkubwa katika jamii kuhakikisha vinapatikana vituo vingi vya watoto kupata elimu zikiwemo huduma kama vile maji shuleni hali ambayo kuhamasisha watoto kupenda kwenda shule  kutokana na mazingira hayo ya kusomea kuboreshwa na kuwa rafiki kwa wanafunzi hao.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI