Sunday, October 16, 2016

NYUMBA 44 ZAEZULIWA NA UPEPO MKALI MUSOMA

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO

WAKATI Wahanga wa tetemeko mkoani Kagera wakiendelea kupatiwa misaada sambamba na harakati za kuwajengea nyumba,Upepo mkali ukiambatana na mvua umeezua nyumba 44 katika Kijiji cha Kiemba Kata ya Ifulifu, Wilaya ya Musoma mkoani Mara. 
 
 Tukio hilo limeendeleza simanzi kwa Watanzania,huku likikwamisha mipango ya maendeleo kwa baadhi ya wakazi waliokumbwa na kadhia hiyo,ambao watalazimika kujipanga upya kutekeleza mipango yao ya kukuza kipato chao na Taifa kwa ujumla.

Katika tukio hilo la Musoma,nyumba  tano,kati ya 44 ziliathirika vibaya kiasi cha kusababisha wamiliki wake kulala nje. Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alikagua baadhi ya nyumba zilizoathirika ili kuona athari za uharibifu huo. 

Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dk Vicent Naano na viongozi wa halmashauri, walitembelea eneo hilo baada ya kupata taarifa za athari za kuezuliwa paa na kuagiza tathmini ifanyike ili Serikali iweze kutoa msaada kwa wananchi hao. 

Profesa Muhongo aliwaambia waathirika hao kuwa Serikali ya Rais John Magufuli ipo pamoja nao na ametumwa kuwapa pole kutoka kwa viongozi wa juu wa Serikali,kutokana na kuathirika kwa nyumba zao kuezuliwa paa na upepo.

Profesa Muhongo aliwaelekeza viongozi wa kijiji hicho wahakikishe wanafanya tathmini ya kweli kwa kupita kila nyumba iliyoathirika na yoyote atakayegundulika amedanganya ili Serikali imlipe, zoezi zima litaahirishwa na kurudiwa upya, pia wahusika watachukuliwa hatua za kinidhamu. 

Aliwaahidi wananchi hao kuanza kupewa misaada baada ya kikao cha halmashauri kupitia taarifa ya tathmini kesho, na kuwaelekeza viongozi kufanya kazi hiyo kwa haraka. 

Profesa Muhongo alikuwa mkoani Mara kwa ziara ya kikazi ya kukagua umeme na kushiriki maadhimisho ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere iliyofanyika nyumbani kwake Butiama juzi.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI