Wednesday, October 5, 2016

WAASWA KUTOJIHUSISHA NA UTOAJI WA MIMBA

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO



VITUO vya afya vinavyomilikiwa na Watu binafsi,vimeaswa kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia taratibu na maadili ya sekta ya afya,na kuhakikisha wanatoa kodi zao kwa wakati ili kuleta maendeleo kwa Taifa.

Aidha vimetakiwa kuhakikisha vinatimiza wajibu kwa umma kadri vibali vyao vinavyoelekeza na kuepuka vitendo vya utoaji mimba kwa jamii  ,ambavyo vinakiuka sheria na utamaduni na wa nchi kwa kulitia doa Taifa.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru,George Mbijima,alitoa onyo hilo wakati akifungua kituo cha Afya cha Kwema kilichopo Kata ya Nyasubi katika Halmashauri ya Mji wa Kahama  kinachomilikiwa na mtu binafsi,kwa kuasa itoe huduma kwa kuzingatia kanuni,taratibu na sheria za afya nchini.

Wamiliki wa vituo vya Afya Binafsi Wilayani Kahama wametakiwa kuacha kujihusisha na utoaji mimba kwenye vituo vyao kwani hali hiyo ni hatari na ni kinyume cha taratibu ya vibari wanavyopewa na serikali kwa ajili ya kufanya shughuli za kuhudumia wananchi.

Mbijima alionya Serikali haitosita kuwachukulia hatua kali za kisheria wadau wa sekta za Afya ambao wanakiuka utoaji huduma stahiki kwa wananchi kwa kushiriki tabia za utoaji mimba kwa lengo la kujiongezea kipato,kwakuwa hayo hayakuwa malengo ya serikali kutoa vibali kwa watu binafsi kumiliki vituo vya afya.

Alikumbusha kuwa lengo la serikali kutoa vibali ni kusaidia huduma za Afya kwa wananchi,hivyo ni vyema wakazingatia weledi wa taaluma hiyo sambamba na kuhakikisha wanalipa kodi stahiki kwa wakati   kwa ajili ya maendeleo ya nchi,na kuhakikisha wanaajili watumishi wenye taaluma na kuwapatia maslahi pasipo vikwazo.

Kiongozi huyo wa mbio za mwenge,alitumia fursa hiyo kuwashawishi wanafunzi kupenda masomo ya sayansi na kuyasoma kwa bidii kusudi wapate kusaidia kuondoa  ombwe linaloikabili sekta ya afya nchini ya ukosefu wa wauguzi na waganga.

Katika taarifa yake Mkurugenzi wa kituo cha Afya cha Kwema Pauline Mathayo alisema mradi huo uliogharimu Shilingi Milioni 578 utahudumia wananchi wanaozunguka Kata ya Nyasubi wapatao 24,217 ambapo kati yake wanawake wenye umri wa kuzaa Elfu tano mia tatu Ishirini.

Mathayo alisema mbali na wanawake hao wajawazito pia kitahudumia idadi kama hiyo kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano,ambapo pia kutakuwepo huduma kwa wanachama wa Bima ya Afya ambapo wamejipanga kw kumudu kutoa huduma ya vipimo vyote vya kisasa katika maisha ya binadamu.


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kahama,Fadhili Nkuru alimwambia kiongozi  wa mbio za mwenge kwamba  utatembele miradi tisa yenye thamani ya Shilingi 1,891,708,722/- katika Halmashauri ya Mji,na baada ya hapo utakimbizwa katika Halmashauri mbili za Msalala na Ushetu.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI