Monday, October 10, 2016

MITANDAO INAATHIRI UCHUMI WA TAIFA.

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO



SERIKALI ya awamu ya tano,imedhamiria kuifikisha nchi katika uchumi wa kati,ambao ni wa viwanda,lakini dunia kuwa kijiji kimoja,kutokana na mabadiliko ya teknolojia  na uwepo wa mitandao,inayotumiwa vibaya na vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa,inatishia kuathiri uchumi wa taifa.

JAMII imeaswa kubadilika kwa kuhakikisha inapambana kwa nguvu na mmomonyoko wa maadili unaochagizwa na maendeleo ya teknolojia na utandawazi,kwa kuitumia mitandao kwa faida ili kufanikisha nchi kuelekea katika uchumi wa kati.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Rocken Hill Academy,Alexander Kazimil,inayomiliki shule za Msingi za Rocken Hill Academy na Rocken Hill Junior pamoja na Shule ya Sekondari ya Anderlek Ridges,katika mahafari ya nane ya kidato cha nne,ya sekondari yake kwa kuitaka jamii ishikamane kulinda maadili ya nchi.

Kazimil alisema wakati nchi ina mkakati wa kuelekea katika uchumi wa nchi,jamii itambue vijana wengi wameathiriwa na matumizi ya mitandao,katika masuala ambayo hayana tija zaidi ya kuharibu maadili ya Kitanzania, na kudai hali hiyo ikifumbiwa macho italikwaza taifa kufikia malengo tarajiwa.

“Matumizi ya mitandao kwa watoto imeathiri uwekezaji na utoaji elimu,kwani badala ya  kujikita katika programu zenye tija,zitakazo kuwa na faida kielimu na hapo badaye kusaidia kukuza uchumi wa nchi,wanajitumbikiza kufuatilia mambo ya anasa,”alisema Kazimil.

Alisema hivyo wazazi,walezi na jamii kwa ujumla  wanawajibu   kuwa karibu na vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa,kwa kuwaelekeza,kuwashauri na kuwaonya juu ya matumizi mabaya ya mitandao ili kujenga Taifa lenye maadili,hatua itakayosaidia uwajibikaji uliotukuka na kufanikisha kufikia uchumi wa kati.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika mahafari hayo,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga,Muliro Muliro,alisema vijana hawana budi kutumia fursa ya muda kwa kuhakikisha wanapata maarifa wanapokuwa shuleni,huku wakitumia mitandao kujikita katika programu zitakazowapatia faida.

Kaonya vijana kutumia muda mwingi katika mitandao katika masuala ambayo hayana faida kiasi cha kuwatumbukiza katika masuala ya makosa mitandao,huku akiwasihi wahitimu kuepuka kujiunga katika vikundi vya vijana wanaotumia madawa ya kulevya,bali wakapambane na vitendo hivyo kwa faida ya nchi.

Awali Mkuuwa Shule ya Sekondari ya Anderlek Ridges,Adamu Lui,aliitaka jamii kushikamana katika suala la malezi, hatua itakayorejesha misingi bora ya maadili ya Taifa inayoathiriwa na utandawazi,kwa kuwekeza katika elimu,na kutambua wajibu wa kushirikiana na walimu katika maendeleo ya masomo kwa mwanafunzi sambamba na kusimamia maadili ya Taifa.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI