Monday, October 17, 2016

DIAMOND PLATINUMZ AMUIBUA SAIDA KAROLI.

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO



NASSIB Abdul,almaarufu;Diamond Platinumz,mkali wa Bongo Fleva,ameurudia kwa umahiri wimbo wa Maria Salome,uliompatia
umaarufu mkubwa,Saida Karoli.

Wimbo huo ;Maria Salome,ulimuibua miaka ya 2000;Saida Karoli,kutokana na tungo yake maridhawa na kuendelea kutoa tungo zingine zenye maudhui ya muziki wa asili,uliokuwa wa aina yake,wenye miondoko ya Kabila la Wahaya,na kumpatia umaarufu,katika Ukanda wa nchi za Afrika Mashariki,anaandika Tatu Mwinyi.

Mkongwe huyo wa nyimbo za asili,katika enzi za kilele cha mafanikio,alikuwa katika uangalizi wa FM Studio,chini ya Ukurugenzi wa Felician Muta,enzi zake zilionekana kufikia tamati baada ya mvumo uliotikisa kila pembe,na kwa watu wa makabila yote nchini na Afrika Mashariki,hata kusahaulika.

Lakini hivi karibuni,Diamond Platinumz,kupitia lebo yake ya Wasafi Classic Baby(WCB),wamemuibua na kumrejesha Saida Karoli,katika medani kwa kutumia wimbo Maria Salome,wenye kibwagizo chenye msisimko cha;Chambua kama Karanga.

Diamond Platinumz,ameucheza upya wimbo huo kwa kushirikiana na mmoja wa wasanii katika lebo yake ya WCB,Raimond,kwa ruhusa na makubaliano na Saida,ambaye amekiri kibao hicho kutendewa haki na vijana hao wa kizazi kipya.

Aidha msanii mahiri wa kizazi kipya,Sara Kais “Shaa”,amepongeza kazi hiyo nzuri iliyofanywa na wasanii hao kutoka lebo ya WBC,huku akidai kwa kipindi kirefu alikuwa na wazo la kuufanyia remix wimbo huo,isipokuwa majukumu yalimkwamisha kuonana kwa wakati na Saida.

Shaa anasema, “….Maria Salome,upo kiafrika zaidi,nimefarijika Diamond kuurudia na ameutendea haki,kadri fikra zangu zilivyokuwa zikinituma kuutendea.”

Hata hivyo amebainisha kwamba baada ya wasanii wa WBC kumuwahi anafikiria kutoka kivingine kwa kuangalia kitu kingine.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI