Monday, October 10, 2016

KANISA KAHAMA KUJENGA KITUO CHA KULEA WATOTO NA WAZEE.

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO



TATIZO la watoto wa mitaani,linazidi kushamiri nchini,huku kukiwa na jitihada hasi za serikali kuwakomboa,kutoka katika madhila yanayowakabili katika maisha yao ya kila siku,yanaowakosesha haki zao za msingi ikiwemo elimu.   

Hata hivyo,Kanisa katoliki jimbo la Kahama limeanza mikakati wa ujenzi wa vituo viwili,vya kulea watoto hao wa mitaani pamoja na yatima,ili kuhakikisha wanapata stahiki zao sambamba na kituo cha kulea wazee wasiojiweza,anaandika Paschal Malulu.


Askofu wa jimbo Katoliki la Kahama,Ludovick Minde,alibainisha mpangu huo,wakati wa misa maalumu ya kuwaombea watu wenye ulemavu mbalimbali,wakiwemo albino walemavu wa macho,yatima  na wazee ambayo ilienda sambamba na kupata chakula pamoja.

Askofu Minde alisema Kanisa linatambua changamoto inayowakabili yatima,wazee na watu wenye ulemavu wa viungo mbalimbali,na kuamua kuleta usaidizi kwa kujenga vituo hivyo,kwa kuwaweka pamoja ili kumtambua Mwenyezi Mungu huku wakipatiwa haki zao za msingi.

Alisema kwa kuwaweka pamoja watoto wa mitaani mbali ya kumjua Mwenyezi Mungu,pia itasaidia kuwajenga kisaikolojia na kutambua umuhimu wa elimu,ambayo ndiyo itakuwa msingi mkubwa wa maisha yao,ambapo alithibitisha mpango huo kufanikishwa na mfuko wa jimbo hilo.


Aidha alifafanua kuwa kupitia mapadri kwa ujumla wataunga mkono jitihada hizo na kuongeza kuwa ujenzi huo utaanza ndani ya mwaka huu kwani sasa bado changamoto yakupata eneo ambalo litakuwa salama kwa watu hao ambao watakuwa chini ya uangalizi wa jimbo la Kahama mjini.

Aliwasihi walemavu kukubaliana na changamoto wanazokumbana nazo ikiwa ni sambamba na wao kukubali msaada wanaopatiwa hata ikiwa kidogo kwani kukataa msaada huo ni kukiuka matakwa ya mungu kwani waumini wanatoa kile alichonacho.


Ibada hiyo ilifanyika ikiwa ni maadhimisho wa mwaka wa huruma,na ikifanyika kwa mara ya kwanza katika jimbo hilo na kuwashiriksha watu wa kada hizo na kukamilika kwa kupata chakula cha pamoja.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI