ONYO limetolewa la jamii duniani
kuepuka kuendelea kutumia simu ya kiganjani aina ya Samsung Galaxy Note 7,kwa
madai kuwa zimekuwa zikiripuka hivyo kuweza kusababisha madhara kwa mtumiaji.
Tamko la zuio la matumizi ya simu
hiyo,limetolewa na kampuni ya Kikorea,inayotengeneza simu za Samsung,kwa kuwataka
watumiaji wake kutupa toleo la ‘Galaxy Note 7’, kutokana na kuwepo kwa ripoti
za matukio mengi ya watumiaji wa simu za Samsung kulipukiwa na simu hizo wakati
wa kuchaji.
Kampuni ya Samsung imetoa tamko
rasmi kupitia tovuti yake ikiwataka watumiaji wa simu hizo toleo la ‘Galaxy
Note 7’ duniani kote kuchukua tahadhari na kuacha kabisa kuzitumia wakati
ikiendelea na uchunguzi zaidi.
Taarifa hiyo imeeleza kwamba
inafanya kazi kazi na Mamlaka husika
kufanya uchunguzi kuhusu kuwepo kwa ripoti za matukio yanayohusu Galaxy Note7.
Kwa sabababu Kampuni hiyo suala la usalama kwa wateja kwao ni kipaumbele.
Hivyo
taarifa hiyo ya Samsung imewataka wauzaji wote wa simu hizo duniani kuacha mara
moja kuuza Galaxy Note 7,hadi hapo uchunguzi wao utakapokamilika na
kujiridhisha kuwa hazina madhara.
Majaribio ya betri ya simu ya
Samsung, Galaxy Note 7 yaliyofanywa katika maabara moja nchini Singapore
yalipelekea simu hiyo kulipuka moto.
Hivi karibuni, hata hapa Tanzania,
kumekuwa na ripoti za matukio ya wananchi wengi kudai kuwa wameripukiwa na simu
za Sumsung walipokuwa wanachaji.
Pia, kulikuwa na taarifa ambazo
hazikuthitishwa na Mamlaka kuhusu watu kulipukiwa na simu hizo walipozipokea
wakati zikiwa kwenye chaji.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI