WATANZANIA waishio
vijijini wametakiwa kujiunga kwenye vikundi vya ujasiriamali ili wapate
Sh.Milioni 50 za miradi ya maendeleo katika kila Kijiji zitakazotolewa na Serikali.
Ushauri huo umetolewa na Afisa
Maendeleo ya Kata ya Isaka,Grace Nyahonge, katika Mkutano wa Hadhara kwa kuwahadharisha kutopata fedha hizo
zinazotokana na ahadi ya Rais John Magufuli,iwapo hawatakidhi vigezo.
Nae Diwani wa Kata
hiyo,Dk.Gerald Mwanzia,amewaasa kabla ya kupata mikopo hiyo ni vyema wakajikita
katika shughuli za ujasiriamali,na kutumia fedha hizo kuendeleza mitaji yao ili
kupata ufanisi wa biashara zao.
Aidha Dk.Mwanzia ameiomba
jamii izingatie kanuni za afya katika kuboresha afya zao na kuwa makini na kuhakikisha
wanatunza mazingira wanayoishi vyema kusudi kuepuka uwezekano wa kupata magonjwa
ya milipuko.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI