MGODI wa Dhahabu wa
Bulyanhulu,unaomilikiwa na Kampuni ya Acacia,huenda ukasaidia kwa kiwango
kikubwa tatizo la kujifungua wajawazito kwa Wakunga wa Jadi,kutokana na
ufadhili uliotoa wa Shilingi Milioni 440 kwa Taasisi ya Benjamin Mkapa,ili
kuboresha huduma ya Afya ya mama na mtoto.
Aidha imefahamika katika
Halmashauri ya wilaya ya Msalala,asilimia 46 ya akina mama wajawazito,hujifungulia
nyumbani wakihudumiwa na wakunga wa jadi,kutokana
na halmashauri hiyo kutokuwa na hospitali ya wilaya,hivyo kuwa sababu ya
kutokea vifo vya akina mama hao na watoto wanaojifungua.
Mganga
Mkuu wa Hospitali ya Halmashauri ya Msalala,Dk.Hamadi Nyembea,anabainisha hali
hiyo wakati wa utiaji saini makubaliano
ya TSH 440 Milioni baina ya Taasisi ya Benjamin Mkapa(BMF)na Mgodi wa dhahabu
wa Bulyanhulu, kwa ajili ya mradi wa kuboresha huduma za afya ya uzazi wa mama na mtoto.
Mgodi
wa Dhahabu wa Bulyanhulu unaomilikiwa na Kampuni ya Acacia,umetia saini hati
hiyo ya makubaliano baina yake na BMF,kutekeleza mradi huo kwa miaka miwili,ambapo,Dk.Nyembea
alifahamisha hatua itakayosaidia kupata vituo bora vya afya katika Halmashauri
ya Msalala,na kusaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto.
“Halmashauri
ya wilaya ya Msalala,hatuna hospitali isipokuwa na tuna vituo vichache vya Afya
ambavyo vipo mbali na jamii kutokana na miundo mbinu ilivyo,na kulazimika
kujifungulia kwa wakunga,na kusababisha kutokea kwa vifo,kuwepo mradi huu
utasaidia kuboresha vituo vya afya ambavyo vitatoa huduma ya upasuaji wa
dharura na kusaidia kupunguza vifo hivyo,”alisema Dk.Nyembea.
Kwa
upande wake Mkuu wa wilaya ya Kahama,Vita Kawawa,alisema ufadhili huo wa Mgodi
wa Bulyanhulu kwa Taasisi ya Benjamin Mkapa,utasaidia kwa kiwango kikubwa
kuboresha huduma ya afya,kwa taasisi hiyo kutoa huduma ya afya moja kwa moja
kwa wananchi walio pembezoni katika Halmashauri ya Msalala,kwa kuwaboreshea
miundo mbinu na kusomesha wataalamu.
Nae
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Benjamin Mkapa,Dk.Ellen Mkondya Senkoro,alisema
taasisi yake inafanya kazi na serikali,ikiwa na lengo kubwa la kusaidia mkakati
wa serikali,ambapo kupitia mradi huo wanatarajia kusaidia suala la miundo mbinu
na wataalamu katika zahanati ya Kakola na Kituo cha Afya Cha Bugarama,ili kupunguza
vifo vya mama na mtoto.
Meneja
Mgodi wa Bulyanhulu,Graham Crew,alisema mgodi wake kupitia Mfuko wa Maendeleo
umekuwa ukitoa ufadhili mbalimbali wa shughuli za Kijamii katika eneo
linalozunguka mgodi huo na kupitia ufadhili walitoa utasaidia mapambano ya Ukimwi
na kuboresha afya ya mama na mtoto,ambao ana imani mradi huo utatekelezwa kwa
ufasaha na Mfuko huo wa Benjamin Mkapa.
MENEJA Mgodi wa dhahabu Bulyanhulu,Graham Crew na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Benjamini Mkapa,Dk.Ellen Senkoro,wakisaini Mkataba. |
Akizungumzia
Ufadhili huo,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala,Patrck
Kalangwa,alisema pindi mradi huo utanufaisha wananchi zaidi ya 321,852 katika
Halmashauri ya Msalala,kutokana na kusaidia kuondoa changamoto zinazokabili kwa
kipindi hiki,ikiwemo nusu ya wajawazito kujifungulia nyumbani na kutopatikana
huduma ya upasuaji wa dharura.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI