TAMKO LA UMOJA WA KLABU ZA WAANDISHI
WA HABARI TANZANIA JUU YA KUTEKWA KWA MWANDISHI WA HABARI WA SAUTI YA UJERUMANI
( DW ) SALMA SAID.
Salma Said mwandishi wa DW
Zanzibar ametoweka baada ya kutekwa na watu ambao hawajafahamika jijini Dar es
salaam, hali ambayo imeleta fadhaa na mshtuko kwa waandishi, jamii na familia
yake hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa marejeo Zanzibar.
Ifahamike kuwa Kazi ya
mwandishi wa habari ni kutoa habari juu ya kila kinachoendelea katika jamii ,
hivyo kama kuna dosari , dosari hiyo ni ya jamii na sio ya anayeieleza dosari .
UTPC inalaani na kupinga
utekaji uliofanywa ambao sababu zake bado hazijulikani, hivyo tunaitaka
serikali kuhakikisha Salma Said anatafutwa, kupatikana na anaachiwa huru mara
moja kwa kuwa Serikali ndio yenye jukumu la kulinda raia wake.
Kama utekwaji wa Salma
umefanywa kutokana na kazi yake ya uandishi habari tunalaani vikali hatua hiyo,
vitendo hivi havipaswi kuendelea katika nchi inayoheshimu misingi haki na
Demokrasia, Vitendo vya namna hii vinadumaza na kufifisha uhuru wa habari
.
Tunapinga kwa nguvu zetu zote
waandishi wa habari kukamatwa na vyombo vya dola au makundi ya kihalifu kwa
visingizio ama vya uchochezi au maslahi ya taifa.
Waandishi tutaendelea kufanya
kazi zetu bila kujali vitisho vya aina yoyote ile kutoka kwa mtu yoyote au
Serikali.
Imetolewa na DEOGRATIUS NSOKOLO RAIS WA KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA -UTPC. March 19, 2016
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI
Imetolewa na DEOGRATIUS NSOKOLO RAIS WA KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA -UTPC. March 19, 2016