Saturday, March 19, 2016

JPM ATEUA WAKURUGENZI WA TBC,NSSF,RAHCO

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa watendaji wakuu wa Taasisi tatu za serikali kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo.


Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, Ikulu; Gerson Msigwa,alisema Rais Dkt. John Pombe Magufuli,alianza kwa kumteua Profesa Godius Kahyarara, kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF).


Msigwa alisema Uteuzi huo umefanyika kwa mujibu wa Sheria ya NSSF namba 28 ya Mwaka 1997, Kifungu cha 42, kinachoeleza kuwa Rais ndiye mwenye mamlaka ya kuteua Mkurugenzi Mkuu wa NSSF.


Prof. Kahyarara anachukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Ramadhan Dau, ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.


Aidha Msigwa alisema Rais Dkt. John Pombe Magufuli,baada ya kufanya uteuzi huo aligeukia  Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).
ambapo alimteua Dkt. Ayub Rioba Chacha kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo.


Dkt. Rioba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Clement Mshana ambaye amestaafu.


Aliendelea kusema kwamba,Rais Dkt. John Pombe Magufuli alikamilisha uteuzi wake kwa kumteua Dkt. Mussa Iddi Mgwatu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania (RAHCO).


Dkt. Mgwatu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi Benhadard Tito, ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

 


 
 

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI