Sunday, March 27, 2016

MGODI WA DHAHABU BULYA WAKABIDHI HALMASHAURI MILIONI 700.DC KAHAMA AONYA.

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO





MKUU wa wilaya ya Kahama,Vita Kawawa,ameonya kuwawajibisha na kuwachukulia hatua kali za kisheria watendaji katika Halmashauri ya Msalala,watakaobainika kufuja na kuzifanyia ufisadi,fedha za mrahaba zinazotolewa kama ushuru wa huduma na Mwekezaji wa ACACIA,kupitia Mgodi wake wa Dhahabu wa Bulyanhulu.MENEJA Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu,Graham Crew akiongea na Mkuu wa wilaya ya Kahama Vita Kawawa.
 

Mgodi wa Bulyanhulu umeipatia  Msalala kiasi cha Shilingi Milioni 714.8 Halmashauri ya Msalala zikiwa ni Ushuru wa huduma unaostahili kupatiwa Halmashauri hiyo kutokana na kufanya kazi za uchimbaji dhahabu katika eneo lake.


MENEJA Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu,unaomilikiwa na Kampuni ya ACACIA,Graham Crew,akimkabidhi mfano wa Hundi,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala,Patrick Karangwa,katikati yao ni Mkuu wa wilaya ya Kahama,Vita Kawawa na aliye pembeni kwa Karangwa ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala,Mibako Mabubu.


Mkuu huyo wa Wilaya,Kawawa alimwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala,Patrick Karangwa kuhakikisha  fedha hizo zilizotolewa na Mgodi kwa ajili ya ushuru wa huduma zinatumika vyema katika miradi yenye tija inayoonekanakatika jamii.
MENEJA Ufanisi wa Mgodi wa Bulyanhulu,Elias Kasitila,akionesha ramani ya machimbo ya Mgodi.



 “….sitaki masuala ya kusema unajua pesa tuliitumia katika kuweka kifusi barabarani na sasa mvua imekiosha, hapana, hilo litakuwa ni jipu litatakiwa kutumbuliwa, fedha hizi zitumike kujenga miradi inayoonekana kama vile vyumba vya madarasa, zahanati nakadhalika.”alisema Kawawa.
MKUU wa wilaya ya Kahama,Vita Kawawa.


Aidha aliagiza uongozi wa Mgodi kuhakikisha unaipatia Halmashauri ya Msalala,orodha ya makampuni yanayofanya kazi na mgodi huo kutokana nayo kustahili kulipa ushuru huo kwakuwa yanafanya kazi katika eneo la Halmashauri hiyo lakini yamekuwa yakikaidi.
 
MKUU wa wilaya ya Kahama,Vita Kawawa,akiongoza msafara kushuka katika Lifti iliyowafikisha eneo la machimbo.



Kwa upande wake Meneja mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu,Graham Crew,alisema pindi fedha hizo zikitumika kwa uadirifu zitasukuma maendeleo katika Halmashauri hiyo,na kuwafanya wananchi kuona faida ya uwepo wa Mwekezaji huyo.
MWENYEKITI wa Halmashauri ya Msalala,Mibako Mabubu akiongea.


Nae Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo,Karangwa,alihakikisha kuzisimamia vyema fedha hizo na kuuomba mgodi huo kujitoa kwa nguvu katika kuchangia shughuli zingine za maendeleo zilizoibuliwa na wananchi katika katika Kata za Karibu na Mgodi huo na halmashauri yote kwa ujumla.
MKUU wa wilaya Kahama,Vita Kawawa akiongea machimboni.

Wakati mkuu huyo wa wilaya akitoa onyo hilo,katika Halmashauri ya Mji wa Kahama fedha kama hizo zilizotolewa na Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi zilitumika kifisadi,na kusababisa kuunda Kamati iliyoibua uozo huo na kusababisha watumishi watano kutimuliwa kazi huku wengine wakipewa onyo na kukatwa mishahara yao.

picha zaidi:-.............
 

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI