KATIKA kuteleza zoezi la
uhakiki wa silaha mkoani Arusha,umewezesha kupatikana kwa bunduki zaidi ya 100
zilizokuwa zikimilikwa na wananchi kinyume
cha sheria huku miongoni mwake zikiwemo sita za kivita, katika eneo la Loliondo,wilayani
Ngorongoro.
MKUU wa wilaya ya Ngorongoro,Hashimu Shaibu Mgandila. |
Mkuu wa wilaya ya
Ngorongoro,Hashimu Mgandila,alisema katika zoezi hilo lililofanyika kwa kipindi
cha mwezi mmoja wamefanikiwa kupata silaha za kivita sita,zilizonunuliwa
kienyeji na kumilikiwa kinyume cha sheria na wananchi.
Aidha alisema mbali na
silaha hizo zilizokuwa zikimilikiwa kinyume cha sheria pia kuna baadhi yake zilizokuwa
zikimilikiwa kihalali,lakini imelazimika kuzishikilia kutokana na hofu iliyopo
juu ya matumizi yake kama ni sahihi,hivyo kulazimika kuwahoji wamiliki wake na
pindi wakijiridhisha watawarejeshea wamiliki wake.
MKUU wa wilaya ya Ngorongoro. |
Zoezi la kuhakiki silaha
ni maelekezo yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Daud Ntibenga,linalolenga
kudhibiti matumizi mabaya ya ongezeko la silaha ambazo zimekuwa zikitumika
kufanyia uhalifu na kuua wananchi wasio na hatia.
Mkoa wa Arusha unatajwa
kuwa ni miongoni mwa mikoa yenye watu
wengi wanaomiliki silaha,ingawa baadhi yake kuwa na vibali vya umiliki lakini
upatikanaji wake na matumizi yake,vinadaiwa
kuwa na utata.