SIMBA
Sports Club imerejea kileleni mwa Ligi Kuu Bara kwa kuitwanga Ndanda FC kwa
mabao 3-0 katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,huku
mshambuliaji wake Hamis Kiiza akivuka rekodi ya ufungaji magoli iliyowekwa na
kinara wa mabao msimu uliopita.
Magoli
ya Simba Sport katika mchezo wa jana uliochezwa Jijini Dar Es Salaam bao la
kwanza lilipachikwa mnamo dakika ya 36 ya Mchezo na Mwinyi Kazimoto kwa shuti
kali baada ya kuunganisha krosi safi ya Hassan
Kessy.
Mnamo
Dakika 57 kona safi ya Ajib,inatendewa haki na Hamis Kiiza aliyeruka juu kabisa
na kupiga kichwa cha kiufundi kabisa na mpira kutinga nyavuni,kabla ya dakika
ya 72 kuifungia bao la tatu, ni baada ya shuti kali la Majabvi, kipa wa Ndanda kulitema
na Lyanga kuuwahi mpira na kutoa pasi
safi kwa Kiiza.
Kiiza
amefunga mabao mawili wakati Simba ikiiangusha Ndanda FC kwa mabao 3-0, sasa
amefikisha mabao 18 huku Tambwe akiwa na mabao 17 hivyo kuweza kukaa kileleni
katika ufungaji bora na kuvuka rekodi iliyowekwa msimu uliopita na kinara wa
upachikaji mabao,Simon Msuva.
Tambwe
alikuwa mshambuliaji aliyefikisha bao 17 na kufikia rekodi ya Msuva baada ya
Yanga kuitwanga African Sports kwa mabao 5-0 huku akifunga mawili na kumpita Kiiza aliyekuwa na
16 wakati yeye alikuwa na 15.
Kiiza
raia wa Uganda na Tambwe kutoka Burundi wamekuwa wakichuana kwa kasi kubwa katika
ufungaji wa mabao,huku kukiwa hakuna uhakika kati yao atakayeibuka mfungaji
bora msimu huu ama ataibuka mshambuliaji mwingine kuwapita na kutwaa kiatu
hicho cha ufungaji bora.
Jijini
Mbeya katika uwanja wa Sokoine timu ya Mbeya City ilipata ushindi wake wa sita
katika Ligi Kuu Bara baada ya kuishinda Stand United kwa mabao 2-0.
Hadi
timu zinakwenda mapumziko,wenyeji Mbeya City walikuwa
wakiongoza kwa bao moja lililofungwa na Raphael Alfa.Kipindi cha pili kilianza
kwa Stand United kucheza kwa kasi kutaka kusawazisha,lakini walikatishwa tamaa
baada ya kupachikwa bao la pili lilifungwa na Ramadhani Shamte.
Kwa
ushindi huo, Mbeya City sasa wamefikisha pointi 24 na kupanda hadi nafasi ya
nane wakitoka nafasi ya 10.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI