Wednesday, March 9, 2016

YOUNG AFRICANS YATEMBEZA KICHAPO,TAMBWE NOMA!

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO



MABINGWA watetezi wa Ligi Tanzania Bara,Young Africans wamedhihirisha hawana mchezo zaidi ya kuhakikisha wanatetea taji lao,baada ya jana kutembeza kichapo cha bao  5 - 0  dhidi ya ndugu zao African Sports ya Tanga.
 

Katika mchezo huo uliochezwa jana Jijini Dar Es Salaam,mshambuliaji wa Kimataifa wa timu hiyo Amis Tambwe alionesha kiu yake ya kutwaa Kiatu cha Dhahabu kwa kupachika bao mbili katika Dakika ya 51 na 73,na hivyo kumzidi bao moja mshindani wake wa Karibu Hamisi Kiiza wa Simba.

Mabao mengine ya Dar Young Africans yalifungwa na Kelvin Yondani mnamo dakika  32 ya mchezo,Donard Ngoma dakika ya 40 na Matheo aliyepachika bao la tano katika dakika ya 62.

Kwa ushindi huo Dar Young Africans inaongoza Ligi kwa alama 50 ikifuatiwa na Watani zake Simba Sports Club wenye alama 48 na Azam wenye alama 47 huku wakiwa nyuma kwa mchezo mmoja.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI