RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli, amefanya
ziara ya ghafla,Benki Kuu ya Tanzania “BoT”na
kumuagiza Gavana wa Benki hiyo, Profesa Benno Ndulu, kusitisha mara moja malipo
ya Shilingi Bilioni 925.6,ambayo yalikuwa yameidhinishwa.
Rais Magufuli aliamuru kusitishwa kwa malipo hayo yaliyodaiwa ni malimbikizo ambayo tayari
yalishaidhinishwa (Ex-Checker) na kuamuru yarudishwe Wizara ya Fedha na Uchumi
kufanyiwa uhakiki upya,ambayo BoT ilikuwa katika mchakato wa kufanya malipo.
Kwa mujibu wa Taarifa ya Ikulu iliyotolewa na Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa, Rais pia alimuagiza Gavana wa
benki hiyo kupitia upya orodha ya wafanyakazi wa benki hiyo na kuwaondoa mara
moja wale wote ambao hawana ulazima wa kuwa wafanyakazi wa benki hiyo.
Rais John Magufuli akiteta
jambo na Gavana wa Benki Kuu (BoT), Profesa Benno Ndulu. Kushoto ni Waziri wa
Fedha na Uchumi, Dkt. Philip Mpango.
|
"Haiwezekani tukawa na kundi kubwa la wafanyakazi, wanalipwa
mishahara wakati hata kazi wanazofanya hazijulikani" Rais Magufuli
amenukuliwa katika taarifa hiyo.
Kuhusu usitishwaji wa malipo hayo, taarifa hiyo imesema, Rais
ameagiza wizara ya fedha na Mipango ifanye upya uhakiki wa malipo hayo, ili
kubaini kama walioidhinishwa kulipwa wanastahili kulipwa ama vinginevyo.
Aidha taarifa hiyo imesema, Rais Magufuli ameagiza
kitengo cha madeni ya nje ambacho awali kilikuwa chini ya BoT kabla ya
kuhamishiwa Wizarani, kirejeshwe Benki Kuu mara moja ili kuimarisha udhibiti wa
ukopaji na ulipaji wa madeni.
Maagizo hayo ya Rais, ameyatoa katika mazungumzo yake na
watendaji wakuu wa benki hiyo, wakiongozwa na Gavana Ndulu, Manaibu wake
wawili, Wakurugenzi na Mameneja