MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa
Shinyanga (CCM) ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida,Lucy
Mayenga amedai kumuomba Rais wa awamu ya Tano Dr, John Magufuli kutokumteuwa
tena katika wadhifa huo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kukwama kwa
biasahara zake.
Kauli hiyo aliitoa katika
sherehe za kutimiza miaka 39 ya Chama cha Mapinduzi zilizoandaliwa na
Umoja wa Jumuia ya Wanawake (UWT) Mkoa wa Shinyanga zilizofanyika katika
kata ya Nyamilangano katika Halmashauri ya Ushetu Wilayani hapa.ambapo ilizusha
mjadala,huku baadhi ya wananchi wakidai Mkuu huyo wa wilaya amehofu kutumbuliwa
jipu.
Mayenga alisema kuwa kutokana na
kubanwa kwa shughuli za kibiashara zake anazozifaya pamoja na shughuli za
kibunge katika Mkoa wa Shinyanga ndizo zimepelekea kumwomba kiongozi huyo wa
juu wa Nchi kuachaa kumteuwa kuwa Mkuu wa Wilaya pamoja na vyeo vingine.
“Majukumu yamenizidi,mara ubunge
mara Ukuu wa wilaya huku biashara zangu zinanitazama,nimeona zintowezana na
kasi ya awamu hii,hivyo Niliamua kwenda mpaka kwa Rais John Magufuli na
kumwonyesha nia yangu ya kutotaka tena kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya katika
sehemu yeyote hapa nchini,"alisema
"Na yeye kama Rais aliniambia
kuwa nisubiri mpaka hapo atakapoteuwa tena Wakuu wapya wa Wilaya katika
Serikali yake ya awamu ya Tano”,Aliongeza kusema Lucy Mayenga.
Aidha Mbunge huyo aliendelea kusema
kuwa sio kama yeye ameogopa kutokuwepo katika uteuzi mpya bali ameamua
kwa Ridhaa yake kuacha Nyadhifa hiyo ya Serikali na kuongeza kuwa nguvu kubwa
kwa sasa itakuwa katika kuwatumikia Wananchi kama Mbunge pamoja na shughuli
zake za kibiashara .
Baadhi ya Wanachama
wa Umoja wa Wanawake na Jumuiya ya Wazazi
waliokuwepo katika sherehe hizo wakizungumzia kuhusu kauli ya Mbunge huyo
walisema kuwa ni bora amejua mapema kuwa hawezi kuendana na kasi ya Rais
Magufuli na kuwataka wengine wajitathimini na kubaini kama wana
mapungufu katika utendaji kazi kuachia ngazi mapema.
“Mimi nimefurahia kitendo cha Lucy
Mayenga kuomba mapema kutoteuliwa na Rais Magufuli na Kama kuna viongozi kama
hao wapo ni bora wakawapisha wengine wenye uewezo wa kuongoza Watanzania katika
uongozi wa awamu hii ya tano”, Alisema Selina Mkula Mwanachama wa Jumuia ya
Wazazi.
"huyu dada ametambua hamudu
kuhudumia wananchi katika ngazi ya serikali,na hapana shaka amebaini hayumo
katika uteuzi haingii akilini madai yake hayo,kwani ni lini kakutana na
Magufuli na kumueleza madai hayo hapa anatuongopea huyu katambua ni jipu
linalotakiwa kutumbuliwa na serikali ya awamu ya tano,"alisema Salima
Makoye,mwanachama wa UWT.
Hata hivyo katika Sherehe hizo Umoja
wa Wanawake Mkoa wa Shinyanga ilifanikisha kuwapokea Wanachama wapya 56 hali
ambayo itachangia katika kuikuza Jumuia hiyo ambayo kwa sasa inakabiliwa na
Changamoto nyingi za kuikuza.
Pia katika hatua nyingine Mbunge wa
Jimbo la Ushetu Elias Kwandikwa alitoa Msaada wa Mifuko 50 katika shule tatu
moja ikiwemo ya sekondari na Mbili zikiwa za msingi ili kuinua sekta ya Elimu
katika jimbo hilo jipya Wilayani ushetu.
Mifuko hiyo aliitoa katika
shule ya Sekondari ya Nyamilango ambayo ilipata mifuko 10 huku katika shule ya
Msingi Mitenga na Nyamiliangani ikipta Jumla ya mifuko 20 kila moja hali
iliyofanya jumla ya mifuko ya Saruji iliyotolewa na Mbunge huyo kufikia 50.
Pia Mbunge huyo alihaidi kutoa
Vyerehani 20 kwa makatibu kata wa Umoja wa Jumuia ya Wazazi katika hizo ili
kuhakikisha kuwa waanzanzisha shughuli za vitega uchumi katika kata zao hali
ambayo itachangia katika kuleta maendeleo katika Jumua hiyo.