RAIS wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, ameendelea kupanga
safu yake ya Serikali ya Awamu ya Tano kwa kufanya uteuzi wa wakuu wa mikoa 26
ya Tanzania Bara.
Katika
uteuzi wake huo,Rais Magufuli ameteua Wakuu wa Mikoa wapya 13,huku saba akiwabakiza
katika vituo vyao vya kazi, kati yao watano akiwahamisha vituo vya kazi huku
mmoja akimpangia Mkoa Mpya wa Songwe.
Akitangaza
leo Ikulu Jijini Dar es salaam, Uteuzi huo wa Wakuu wa Mikoa,Kaimu Katibu Mkuu
Kiongozi, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe ,aliwataja walioteuliwa kuwa ni;Paul Makonda anayekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.
Makonda
ametumikia kwa kipindi kifupi wadhifa wa Wakuu wa Wilaya ya Kinondoni,ambapo
hivi karibuni Rais Magufuli akiongea na Wazee wa Dar Es Salaam alimsifu
uwajibikaji wake na kudai isijekuwa nongwa akimteua kuendelea na wadhifa huo
ama kuwa Mkuu wa Mkoa.
Mhandisi
Iyombe aliwataja wengine kuwa ni Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Elias Kyunga anayekuwa
Mkuu wa Mkoa wa Geita. Meja Jenerali
Mstaafu Salum Mustafa Kijuu – Mkuu wa Mkoa wa Kagera. Meja Jenerali Mstaafu
Raphael Muhuga – Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
Pia wamo Brigedia
Jeneral Mstaafu Emmanuel Maganga – Mkuu wa Mkoa wa Kigoma. Godfrey Zambi – Mkuu
wa Mkoa wa Lindi. Steven Kebwe – Mkuu wa Mkoa wa Morogoro. Kamishna Mstaafu wa
Polisi Zerote Steven – Mkuu wa Mkoa wa Rukwa. Anna Malecela Kilango – Mkuu wa
Mkoa wa Shinyanga. Mhandisi Methew Mtigumwe – Mkuu wa Mkoa wa Singida. Antony
Mataka – Mkuu wa Mkoa wa Simiyu. Aggrey Mwanri – Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
Katika
uteuzi huo pia wamo;Martine Shigela – Mkuu wa Mkoa wa Tanga. Jordan Mungire
Rugimbana – Mkuu wa Mkoa Dodoma. Said Meck Sadick – Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.
Magesa Mulongo – Mkuu wa Mkoa Mara. Amos Gabriel Makalla – Mkuu wa Mkoa Mbeya.
John Vianey Mongella – Mkuu wa Mkoa Mwanza.
Wengine
ni Daudi Felix Ntibenda – Mkuu wa Mkoa
wa Arusha. Amina Juma Masenza – Mkuu wa Mkoa wa Iringa. Joel Nkaya Bendera –
Mkuu wa Mkoa wa Manyara. Halima Omary Dendegu – Mkuu wa Mkoa wa Mtwara. Rehema
Nchimbi – Mkuu wa Mkoa wa Njombe.
Pia Mhandisi
Evarist Ndikilo – Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Said Thabit Mwambungu – Mkuu wa Mkoa
Ruvuma,huku Luteni Mstaafu Chiku Galawa akimteua
kuwa Mkuu wa Mkoa mpya wa Songwe.
Kwa
mujibu wa Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano IKULU Gerson Msigwa, wakuu wote wa
mikoa walioteuliwa wataapishwa Jumanne tarehe 15 March 2016 saa 3:30 Asubuhi
Ikulu, Dar es salaam.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI