KUELEKEA Uchaguzi Mkuu wa marudio Zanzibar hapo Machi 20 mwaka huu baada ya kufutwa ule wa Oktoba 25,mwaka jana,tukio la kutia hofu limeibuka baada ya Nyumba nane
kuchomwa moto usiku wa kuamkia jana Kisiwani Pemba.
Miongoni mwa nyumba hizo zimo nyumba za
makazi,tawi la CCM Kibirinzi na kituo cha afya Kiuyu kilichokuwa kinatumika
kuhifadhi dawa zilizokwisha muda wa matumizi na mali za idara ya afya.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi
Mkoa Kaskazini Pemba,Kamishina Msadizi Hasana Nasiri Ali, alisema kufuatia tukio hilo tayari wana
washikilia watu wawili kwa tuhuma ya matukio hayo huku upelelezi mkali ukiwa umeanza ili kubaini wengine.
Nae Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa Kaskaini Pemba, Omar Khamis Othuman alisema
kufatia matukio hayo,wamepiga marufuku watu kuzungumza kwenye
vijiwe kuanzia saa mbili usiku hadi asubuhi.
Wamiliki wa
nyumba zilizo ziliokumbwa na kadhi hiyo na baadhi ya
mashuhuda walisema awali walijihisi joto kali na ghafla wakona moto
unawake juu kwenye paa la nyumba ndipo walipo piga yowe kuomba msada.
Afisa mdhamini wizara
ya afya Pemba Ukasha Daudi Ukasha amesema miongoni mwa hasara zilizo letwa na
moto huo ni kuteketeza vitabu vya kusomea mbali mbali vya shule ya
sekondari kiuyu minungwini walivyo pewa msada vilivyo hifadhiwa ndani ya kituo
hicho.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI