Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe
akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kazuramimba mkoani Kigoma, katika
mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM juzi.
Badhii
ya waliokuwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa serikali ya
kijiji cha Kapalamsenga katika jimbo la Mpanda Vijijini, wakimkabidhi
kadi za CCM Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
Freeman Mbowe, walipoamua kujiunga na Chadema, baada ya mkutano wa
Oparesheni Delete CCM, uliofanyika kijijiniHapo
Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe
akisalimiana na Bi. Mariamu Ramadhani (86), baada ya kuwasili katika
kijiji cha Kapalamsenga mkoani Katavi, ambako alihutubia mkutano wa
hadhara wa Oparesheni Delete CCM
Naibu
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Zanzibar), Salumu
Mwalimu akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kazuramimba mkoani Kigoma,
katika mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM.
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman
Mbowe, amewataka wananchi wa Mkoa wa Kigoma kuijua historia ya mageuzi
ya Mkoa huo ili kuepuka kuwalaumu viongozi wanaosimamia vyama hivyo
pindi wanapochukua maamuzi magumu.
Alisema wananchi wengi wamekuwa wakishabikia na kuwahukumu viongozi
hao bila kuangalia chimbuko la vyama hivyo, vilikotoka na hatimaye
kufikia hatua vilipo sasa hususan katika mkoa huo ambao umekuwa chimbuko
la mabadiliko.
Akijibu swali lililoulizwa na mtu ambaye alijitambulisha kwa jina la
Cheche wa Cheche, katika mkutano wa hadhara wa ‘Oparesheni Delete CCM’,
uliofanyika kwenye kijiji cha Mnanila Manyovu mkoani hapa jana, Mbowe
alisema Mkoa wa Kigoma ulizalisha viongozi wengi maarufu katika mageuzi.
Alisema utumishi ndani ya chama hicho haupimwi kutokana na mtu kutoka
mkoa gani, bali hupimwa kutokana na ujasiri, uwezo wa mtu na kamwe
kiongozi makini hawezi kumpiga vita mtu kwa sababu ya kabila au dini
yake.
Akitoa mfano wa viongozi waliotegemewa na wanachi wa mkoa huo katika
kuendeleza mageuzi, Mbowe, alisema Daniel Nsanzugwanko, Aman Kabourou na
Zitto Kabwe walionyesha umahiri wao katika kuongoza vyama vya siasa
enzi zao kabla ya kurubuniwa na kuvisaliti.
Akifafanua zaidi kuhusu lawama ambazo zimekuwa zikielekezwa kwake na
chama anachokiongoza, hususan kuondolewa kwa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu
wa chama hicho, Zitto Kabwe, Mbowe alisema kuwa kamwe hawezi kumzibia
kwa kuwa ndiye aliyemtafuta na kumuingiza katika siasa akiwa kijana
mdogo.
Labda nilazimike kutoa ufafanuzi huu ili muelewe ukweli wake. Mimi
ndiye nilimwingiza Zitto katika siasa akiwa kijana madogo, nilimwita
akitokea masomoni Ujerumani, kisha nikamshauri akagombee ubunge katika
jimbo la Kigoma Kaskazini, nikampa pesa na gari ambalo mpaka sasa
hajalirudisha,” alifafanua.
Alisema Zitto ndiye aliyetia mchanga kitumbua chake kwa kusaliti
chama kutokana na kukubali kurubuniwa na viongozi wa CCM, jambo ambalo
lisingelivumiliwa ndani na nje ya chama.
Huku akishangiliwa na umati mkubwa uliofurika katika Uwanja wa
Community Centre mjni Kigoma, Mbowe alisema kuwa, atahakikisha
anakilinda chama hicho kwa gharama yoyote bila kumwonea mtu ili
kukijengea imani kwa watanzania.
Akizungumzia usaliti wa aliyewahi kuwa Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia
chama hicho, Dk. Aman Kabourou, alisema kwamba akiwa kijana mwanzilishi
wa chama hicho, alishiriki kikamilifu kumpigania Dk. Kabourou kumleta
nchini na hatimaye kugombea ubunge mwaka 1993 katika uchaguzi mdogo.
“Nyinyi vijana wengi inawezekana hamjui hiki chama kilianza vipi
katika mkoa huu. Mimi nilishiriki kikamilifi kumwezesha Dk. Kabourou
kuwania ubunge wa Kigoma Mjini kwa kutoa nauli ya kumleta kutoka
Uingereza alikokuwa akiishi, yeye na mkewe na pia nikampa pesa
kumwezesha kufanya kampeni, leo hii mnanihukumu Mbowe,” aliongeza.
Alisema kuwa kuna baadhi ya watu wanafikiri kuwa anampiga vita Zitto,
jambo ambalo si kweli kwa kuwa amemlea, amekula na kulala nyumbani
kwake kabla hajakua kiuchumi.
Jana, Mbowe alifanya ziara yake katika jimbo la Manyovu, Kigoma mjini
katika uwanja wa Community Centre Mwanga, Munawila na Mahembe ambako
aliendelea kuwasisitiza wananchi kuwapa dola upinzani kwa kuanzia
uchaguzi wa serikali za mitaa.
CHANZO CHA HABARI NI GAZETI LA TANZANIA DAIMA.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI