JITIHADA za uokoaji zikiendelea.. |
WATU
watano wamefariki Dunia papo hapo akiwamo mmoja ambaye ameuawa eneo la tukio
kwa la ajali iliyosababisha vifo vinne baada ya gari la abiria aina ya Scania
kampuni ya Wibonela lenye namba za
usajili T 412 CGN kuanguka katika Kata ya Nyasubi wilaya ya Kahama mkoani
Shinyanga.WATU wakiishuhudia gari lililopata ajali. |
Akiongea
na Waandishi wa Habari Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya wilaya ya
Kahama;Dkt.Joseph Ngowi alisema katika ajali hiyo watu wanne wamefariki kwa
ajali na mmoja kuuawa kwa kuchomwa na moto,huku 40 wakiwa wamejeruhiwa ambapo
kati yao 26 ni wanaume.
WATU wakishuhudia ajali |
Aidha
alisema katika ajali hiyo mbaya,mmoja wa marehemu hao ni mtoto mdogo wa miezi
mitatu aitwaye aliyekuwa akisafiri na wazazi wake wakitokea wilaya ya Kasulu mkoa
wa Kigoma wakielekea Jijini Dar Es Salaam.
WATU wakizidi kumiminika katika eneo la Ajali. |
Alisema
miongoni mwa marehemu ni mama mjamzito aliyefahamika kwa jina moja la Amina
mwenyeji wa Kigoma na mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Salumu(35-40)
na maiti moja ikishindikana kufahamika
yenye umri kati ya miaka 40 na 45.
NI kipigo kwa Mbaba |
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo walisema
ajali hiyo ilitokea kona ya barabara kuu
ya kuelekea Jijini Dar Es Salaam mkabala wa eneo la Kituo cha mafuta cha Phantom
katika kata ya Nyasubi wakati basi hilo likishindana na mabasi mengine
yanayokwenda mikoani kuwahi katika eneo la mizani ambapo magari hayo hupimwa
uzito.
Mbaba akipokea kipigo cha paka mwizi. |
Mmoja
wa Mashuhuda hao Stansilaus Luhumbika alisema kuwa basi hilo likiwa katika
Mwendo kasi likitokea katika kituo cha mabasi kuingia katika barabara kubwa
ndipo lilipomshida dereva na kuserereka kisha
kubinuka na kuingia katika mtaro,huku matairi yake yakiwa juu.
MBABA hoi kwa kipigo. |
Wakati
huo huo wananchi wenye hasira kali walimuua kwa kumpiga kisha kumchoma moto
kijana mmoja mwendesha bodaboda atambulikanaye kwa jina la Mbaba baada ya kuwaibia
simu,fedha na kompyuta mpakato watu waliokuwa wamejitolea kufanya jitihada za
kuwaokoa waliopatwa na ajali.
KIPIGO kilimpeleka Mbaba katika mtaro. |
Kwa
upande wa majeruhi Dr, Ngowi aliwataja kuwa ni Maulidi Shabani (44) Mkazi wa Ushirombo,
Athumani Isa (21) kazi wa Kahama, Jordani mbeya (28) Mkazi wa Kasulu baba wa
Marehemu Robineck, na Mama wa Marehemu Blandina Patrick (24), Oscar Lameck (19)
Mkazi wa Kigoma, Stamili Shabani (38) Mkazi wa Dodoma, Neema Dustan (18) Mkazi
wa Kahama, Monica Gaston (35) Mkazi wa Nyakato Kahama.
MBABA alipoteketezwa kwa moto. |
Wengine
ni pamoja na Lukas Mlezi (48) ambaye hajulikani anakoishi, Mchungaji Nickson
Andati (34) Mwenyeji wa Nchi jirani ya Rwanda, Joyce Fred (28) Mkazi wa Kahama,
Asnath Remtula (27) Mkazi wa Kahama, Eveline Khamis (6) Mkazi wa Kahama, Happy
Khamis mkazi wa Kahama, Japhet Masha (29) Mkazi wa Kahama, Jackson Elisanto
(26) Mkazi wa Kahama.
Pia wamo Barigerela Ramadhani (40) Mkazi wa Kahama, Rita Bryson (25) Mkazi wa Kahama, Irene Willson ( 17) Mkazi wa Kasulu, John Lembo (45) Mkazi wa Bariadi, Khamis Shabani (31) Mkazi wa Kahama, Emanuel Lumbambo (32) mme wa marehemu Amina mkazi wa Kigoma, Kashindye Masanja (28) mkazi wa Kijiji cha Iponya Kahama, Frank Kishimba, (21) Mkazi wa Isaka Kahama, Peter Bahati ( 22) Mkazi wa Kahama, Iseme Ikila ( 36) Mkazi wa Katoro Geita.
Wamo
pia Ibrani Sanga (30) Mkazi wa Kigoma, Aniku Hamduni (35)Mkazi wa Kahama,
Shabani Omari (16) Mkazi wa Dodoma, Gloria Moses ( 18) Mkazi wa Kahama, Agnes
Groto ( 35) Mkazi wa Ngara, Kurwa Saidi (40) Mkazi wa Kahama, Peter Daudi ( 42)
Mkazi wa Kahama, Tungu Lazaro ( 22) Mkazi wa Bariadi, na Happy David (330 Mkazi
wa Dodoma.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo
na kufika katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama kuwajulia hali Majeruhi
waliokuwepo katika ajali hiyo na kuongeza kuwa Jeshi la Polisi lifanya jitihada
za kumpata Dereva wa Basi hilo Godfrey Prochas ambaye ametoweka kusikojulikana.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI