WITO umetolewa kwa wananchi
kuwa mstari wa mbele kutoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa wahalifu pindi
vinapotokea vitendo
vinavyoashiria uvunjifu wa amani.Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Ernesti Mangu wakati wa kukabidhi zawadi ya shilingi Milioni Kumi kwa watu waliofanikisha kukamatwa watuhumiwa waliovamia kituo cha Polisi Bukombe agost 16 na kuua asikari polisi 2.
Mangu alisema
watu hao waliwataja wahalifu 10 waliofanya uhalifu huo na kukamatwa
pamoja na bunduki zote zilizokuwa zimechukuliwa na amewaomba wananchi wenye
mapenzi mema kutoa taarifa za wahalifu wanapozisikia.
Aliongeza kuwa kutolewa zawadi hizo ni chachu kwa wananchi kuwafichua wahalifu na wataendelea kutoa zawadi kwa wananchi wanaotoa taarifa za kweli za wahalifu na jeshi hilo litazidi kutunza siri zao na kuwahakikishia usalama wao.
Katika
hatua nyingine IGP Mangu aliwataka wamiliki wa magari makubwa yanayosafirisha
abiria kutoajiri madereva wasiokuwa na sifa ili kuepusha ajali za mara kwa mara.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI