Mradi wa barabara ya Kahama Manzese–Kakola, Bulyanhulu, wenye urefu wa kilomita 73, umezalisha ajira 460, huku ukitarajiwa kuchochea uchumi. Anaandika Mwandishi wetu.Msimamizi wa mradi huo, Mhandisi Marco Bee, alisema kuwa ajira 418 zimeenda kwa Watanzania, huku raia wa China wakiwa 42.
Alisema tangu utekelezaji ulipoanza Juni 2024, mradi umeongeza fursa zisizo rasmi kwa mama lishe, wanaohudumia wafanyakazi na kukuza uchumi wao.
Bee alisema kilomita 36 kutoka Kahama Manzese zimekamilika, huku mradi mzima ukitarajiwa kukamilika Desemba 2026 na kurahisisha usafirishaji.

Mhandisi Samson Mgina alisema ujenzi umefikia asilimia 89, huku kilomita 60 zikifanyiwa kazi; mradi ukifadhiliwa na Barrick Bulyanhulu pamoja na Serikali.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI