Wednesday, August 12, 2026

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO

 

MWANAFUNZI AWA MGENI RASMI MAHAFARI YA SEKONDARI.

 

 


Na Ali Lityawi, Kahama.

 

 

TAASISI ya Rocken Hill Academy iliyopo wilayani Kahama, imeandikwa historia ya aina yake baada ya kufanya mahafari ya Shule zake za Msingi na Sekondari, huku Mgeni rasmi akiwa kijana aliyesomea Shule hizo na kupata mafanikio Makubwa.

 

 

Katika mahafari hayo ya 22 kwa Shule za Msingi za Rocken Hill Academy na Rocken Hill Junior, na ya 18 kwa Shule ya Sekondari ya Anderlek Ridges huku Mgeni RASMI akiwa ni mmoja wa wanafunzi waanzilishi wa Shule hizo.

 

 


Mgeni rasmi Dkt Joseph Charles, daktari wa moyo nchini Urusi, amepongeza maendeleo ya shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1999 ikiwa na madarasa mawili, huku yeye akiwa miongoni mwa wanafunzi wa awali, alisema maono, bidii na ujasiri vinaweza kutimiza ndoto.

 

 

"Tunaona hii leo ni mtu mmoja  alikuwa na maono na ujasiri mkubwa sana  hivyo haikuwa rahisi   mara nyingi binadamu huanzia chini  na mwanzo unakuwa mgumu kukutana na vikwazo”amesema dkt Charles, ambaye pia mwaka 2006.alikuwa miongoni mwa wanafunzi waanzilishi wa Shule ya Sekondari ya Anderlek Ridges.

 

 

 Dkt Charles amesema, ".... ukiamini kitu na kukiweka kwenye maono na bidii ya kazi ni  lazima ndoto itimie hivyo ninampongeza mkurugenzi kwa kutokata tamaa na kutimiza  ndoto yake ambayo leo tunaishuhudia."

 

 


Dkt Charles amesema, "Wanafunzi kwa elimu waliyopita  watabadilisha   maisha  kwa kupata  maarifa na sio ufaulu wa mitihani  na  safari yangu ilianza  shule ya msingi Rocken Hill na leo hii nimefika Urusi kama daktari wa magonjwa ya moyo." 

 

 


Dkt Charles amewahasa  wanafunzi waendelee kuwasikiliza walimu na kuwa na bidii ili kuweza kutimiza ndoto zao  na eneo la shule  sio kufaulu mitihani bali linawajengea uwezo wa kwenda kufanya kazi na kulitumikia taifa.

 

 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Rocken Hill Academy, Sir Alexander Kazimil, amewataka vijana kutumia teknolojia ya "akili unde" kama fursa ya kujiajiri, kuongeza kipato na kubuni maisha bora yenye mafanikio zaidi.

 


 

Sir Kazimil amesema hayo katika mahafali ya Shule ya Sekondari ya Anderlek Ridges na Shule za Msingi za Rocken Hill na Rocken Hill Junior zinazomolikiwa na Taasisi ya Rocken Hill Academy zilizopo Mansipaa ya Kahama mkoani Shinyanga, akiwataka vijana kuifahamu dunia ya utandawazi yenye ubunifu, ushindani na fursa nyingi.

 

 


Sir Kazimil amesema dunia ya leo haiwapi nafasi watu dhaifu, wasiojotambua, wazembe, wasio na ndoto wala bidii, hivyo vijana wanapaswa kushindana kimataifa na kutumia ubunifu kujenga maisha yao yenye mafanikio ya kudumu.

 


 

Akieleza safari yake, Sir Kazimil amesema alianza shughuli kadhaa za ujasiriamali huku akifundisha  shuleni, akisisitiza vijana waanzie chini, waweke maono mbele, wafanye bidii na kutumia akili unde kwa maadili na kuepuka tabia potofu.

 

 


Alisisitiza ili ufanikiwe ni budi kuwajibika kwa bidii huku ukilipenda jukumu unaloshughulika nalo na kukuingizia kipato halali na kutokata tamaa, kwani safari ya mafanikio kuna nyakati huwa na vikwazo.

 

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI