Monday, June 5, 2017

WABUNGE WAWILI UPINZANI WAPIGWA STOP KUHUDHURIA VIKAO VYA BUNGE

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO



WABUNGE wa Majimbo ya Kawe na Bunda,kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA );Halima Mdee na Esther Bulaya wamehukumiwa kutohudhuria vikao
vyote vya bunge linaloendelea mpaka mkutano ujao wa Bunge la Bajeti ya 2018/19.

Wabunge hao;Mdee wa Jimbo la Kawe na mwezake Bulaya wa Jimbo la Kawe,wamehukumiwa na  Kamati ya Maadili,katika  Hukumu iliyoungwa mkono na wabunge wengi, waliopitisha azimio hilo kwa kauli ya Kura ya Ndiyooo.

Kamati hiyo  ilidai Bulaya na Mdee wamemaliza adhabu za kawaida zilizopo kwenye kanuni za bunge,ndio maana wameona ni vyema watoe hukumu hiyo.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, George Mkuchika aliliomba Bunge kujadili adhabu inayostahili kulingana na makosa yao. 


Kanuni inasema, mbunge anayefanya kosa la kwanza anaweza akazuiwa kuhudhuria vikao visivyozidi 10 na atayakosea kwa mara ya pili anaweza kuzuiwa kuhudhuria vikao visivyozidi 20.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI