SERIKALI Mkoa wa Shinyanga,imewatoa
hofu Madiwani katika Halmashauri zilizopo mkoani humo,kuwa hawatarejea katika
nafasi zao katika Uchaguzi ujao kwakuwa
itawasimamia,ilimradi wahakikishe
wasaidie Serikali iliyopo madrakani kutimiza ahadi zake.
Hivyo katika kutekeleza hayo wameaswa
kuondokana na kasumaba ya kulazimisha kuwa na miradi mingi katika Kata zao,bali
waelekeze nguvu zao katika kutekeleza miradi michache iliyoibuliwa katika
Halmashauri zao.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Zainabu
Telack,amesema hayo wakati akiongea na Madiwani wa Halmashauri ya
Msalala,wilayani Kahama kwa kuwatoa hofu ya kutochaguliwa Uchaguzi Mkuu
Ujao,badala yake wafanye kazi kwa maslahi ya Halmashauri zao na Serikali
iliyopo madarakani.
Mkuu
huyo wa Mkoa aliwataka Madiwani katika Halmashauri hizo kuondokana na tabia ya
kulazimisha Kata zao kuwa na miradi mingi kwa kigezo itakuwa mkombozi kwao
katika Uchaguzi ujao,hatua inayosababisha kuchelewesha maendeleo ya Halmashauri
husika kutokana na kutokamilika kwa wakati kwa miradi hiyo.
Alisema
kuwepo kwa miradi mingi huku mapato yakishindwa kukidhi kuikamilisha imekuwa
kigezo cha Halmashauri nyingi kuonekana hazijafikisha maendeleo kwa wananchi,na
kusababisha serikali ihukumiwe hivyo kuwataka Madiwani wabadirike kwa kuwa na
mradi mmoja katika kila Kata ambayo itakamilika na kuleta tawsira ya maendeleo
kwa wananchi wao.
Aliwataka
katika kuonesha wanafanya kazi kwa maslahi ya Halmashauri zao,ni vyema pesa
zinazopatikana zikawekwa kipaumbele kukamilisha mradi muhimu kwa Halmashauri
zao,kwa nguvu zote za Madiwani kuzielekeza hapo na kuepuka kasumba kuwa
miaka mitano itakapopita atahukumiwa iwapo Kata yake,haitokuwa na mradi
uliokamilishwa.
“Elekezeni
nguvu kwa kuwa wamoja kukamilisha mradi Kata hadi Kata kwa maslahi ya
Halmashauri,msihofu kutochaguliwa kisa hujaleta maendeleo katika Kata
unayoongoza,tutawasimamia kushinda ilimradi uwe umepigania maendeleo ya
Halmashauri yako kwa ujumla.”Alisema Mkuu huyo wa Mkoa.
Aidha
aliwataka kushikamana na Watendaji wa Serikali katika kufikisha maendeleo
stahiki kwa wananchi huku akiwakumbusha kuwa na utamaduni wa kujibu na kutatua
hoja za wananchi pasipo kuzalisha kero zingine.
Kwa
upande wake Diwani wa Kata ya Isaka,Dr.Gerald Mwanzia ( CCM ),aliahidi
kutoiangusha Serikali ya Awamu ya Tano,kwa kusimamia misingi na miongozo ya
watawala ili kufikisha maendeleo stahiki kwa wananchi,huku wakizingatia sera ya
Hapa Kazi tu.
Nae
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala,Mibako Mabubu,alisisitiza kwa madiwani
kushikamana na watendaji wa Serikali ili kukamilisha hoja mapema zinazotakiwa
na Mkaguzi na Mdhibiti wa Serikali (CAG).
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI