Thursday, June 8, 2017

SHAMBULIO LINGINE PWANI,MGAMBO AJERUHIWA

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO



UHALIFU wa shambulio la kutumia silaha,umeendelea kuibuka katika Mkoa wa Pwani,licha ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini( IGP ),aliyeteuliwa hivi Karibuni,Simon Nyakoro Sirro,kutoa kiapo cha kuhakikisha anaitokomeza hali hiyo,iliyowajengea hofu ya uhai wakazi wa Mkoa huo.

Muendelezo wa matukio hayo yametokea jana baada ya Askari Mgambo, Nurdin Kisinga (33) Mkazi wa Kijiji cha Umwe Kaskazini Ikwiriri, wilayani Rufiji mkoani Pwani,kushambuliwa na kupigwa risasi ya kisogoni na kusababisha kulazwa katika Hospital ya Mchukwi.

Huyu ni mgambo pili kipigwa risasi ndani ya siku mbili baada ya Erick Mwarabu kuuawa juzi saa tisa usiku akiwa uvunguni mwa kitanda chake.

Tukio hilo la Jumatano limetokea katika eneo la Ngomboloni lililopo katika Kijiji cha Umwe Kaskazini ikiwa ni takribani saa 19 tangu Mkuu wa Jeshi la Polisi(IGP), Simon Sirro kufanya mkutano wa mazungumzo na wazee wa wilaya za Kibiti na Rufiji ili kukomesha mauaji katika wilaya hizo.

Akielezea jinsi tukio hilo lilivyotokea, kaka wa majeruhi aliyejitambulisha kwa jina la Kisinga Athumani Kisinga akiwa katika Hospitali ya Mchukwi alisema ndugu yake alipigwa risasi akiwa shambani kwake.

Alisema Nurdin alikuwa akivuna ufuta wake shambani kwake ndipo watu ambao hawajajulikana idadi yao walimpiga risasi moja ya kisogoni na kutokomea kusikojulikana.

Kisinga alisema Nurdin alikuwa ameambatana na vijana wawili ambao ni watoto wake kuvuna ufuta huo.

Alisema mara baada ya kuanguka chini wadogo zake waliomba msaada kwa kupiga yowe na ndipo mtu mmoja alifika eneo la tukio na kumchukua kwa baiskeli hadi barabarani.

Alisema mara baada ya kufika barabarani alifanikiwa kubebwa kwa pikipiki hadi kituo cha Polisi Ikwiriri.

Alifafanua kuwa baada ya hapo alikimbizwa katika kitio cha Afya Ikwiriri ambapo alipatia huduma ya kwanza kituoni hapo na baadaye alipelekwa Mchukwi kwa matibabu zaidi.

Mganga wa zamu katika hospitali hiyo Emmanuel Humbi alisema mara baada ya kumpokea majeruhi huyo,hima walimpeleka kwenye chumba cha X Ray kwa ajili ya uchunguzi,kabla hawajaanza kumpatia matibabu.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI