Tuesday, June 20, 2017

SERIKALI YAOMBA RADHI POLISI KUPIGA WENYE ULEMAVU

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO



SERIKALI imeomba radhi kwa Watanzania wenye ulemavu,kufuatia Jeshi la Polisi,kuwadhibiti kwa kipigo,huku ikiahidi kuwachukulia hatua za kisheria askari waliohusika kuwafanyia vitendo vya kikatiri Walemavu hao.
 
Waziri wa Mambo ya ndani na Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi Mkoani Singida, Mwigulu Nchemba leo bungeni amefunguka na kuomba radhi dhidi ya vitendo vya jeshi la polisi kutumia nguvu kubwa kupambana na watu wenye ulemavu.

Mwigulu Nchemba amekiri kuwa jeshi la polisi lilitumia nguvu kubwa mno kwa watu hao na kusema serikali wamepokea jambo hilo na kuahidi kulifanyia kazi ili siku nyingine lisijirudie.

Anasema,"Kwanza naomba niombe radhi kwa jambo hili na naomba salamu zangu ziwafikie watu wenye ulemavu, ni kweli kwamba kwa kuzingatia hali yao, Jeshi la polisi lilitumia nguvu kubwa."
 
"... ila sisi kama serikali tumeshawasiliana na TAMISEMI na kuzungumza nao juu ya mambo yao, lakini pia tumepokea jambo hili na tunalifanyia kazi ili siku nyingine jambo hili lisijirudie." Anasema Nchemba.
 
Mnamo tarehe 16, Juni, 2017 jijini Dar es Salaam jeshi la polisi lilitumia nguvu kubwa ikiwepo kuwapiga na kuwadhalilisha watu wenye ulemavu ambao walikuwa wamejikusanya katika barabara ya Sokoine, Posta Jijini Dar es salaam ili kwenda kumuona Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala.
 
Watu hao wenye ulemavu walikuwa na lengo la kuwasilisha malalamiko dhidi ya askari wa usalama wa barabarani kuwakamata na kuwazuia kuingia katika jiji. Lakini pia walikuwa wakipigania haki yao ya kuwa na maeneo ya kuegesha vifaa vyao katikati ya jiji.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI