Tuesday, June 20, 2017

MSIBA JANGWANI,ALLY YANGA AFARIKI DUNIA

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO


NI Simanzi na huzuni kubwa umeupata familia ya soka nchini,hususani Klabu ya Dar Young African,kuondokewa na shabiki
wake,mpenzi wake na Mhamasishaji mwenye vibweka vya aina yake,Ally Mohammed,kufariki dunia.

Shabiki huyo amekumbwa na umauti huo  katika ajali ya gari eneo la kijiji cha Chipogoro wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma. 
 
Kifo cha shabiki huyo kimepokewa kwa majonzi na masikitiko makubwa na Uongozi wa klabu ya Yanga SC kufuatia taarifa ya kifo cha aliyekuwa shabiki wao mkubwa aliyefahamika kwa jina la Ally Yanga.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma Lazaro Mambosasa amethibitisha kifo cha aliyekuwa shabiki maarufu wa klabu ya soka ya Yanga Ally Yanga kilichotokea leo katika ajali ya gari aina ya Rav4.

Katika taarifa iliyotolewa na klabu hiyo imesema kifo cha shabiki huyo kimeacha pengo kubwa kwa nafasi yake ambayo ilipelekea kujipatia umaarufu mkubwa pamoja na kuwa balozi mzuri kama mwanachama wa timu hiyo.

Enzi za uhai wake Ally Yanga atakumbukwa kutokana na mbwembwe zake alizokuwa akizionesha za kujipaka masizi ya mkaa usoni pindi klabu ya Yanga ikiwa uwanjani.

 Ally Yanga ambaye pia ni mkereketwa wa Mwenge wa Uhuru alikutwa na mauti akiwa katika gari la kampuni ya Faidika ambalo lilikuwa kwenye shughuli zake za promosheni na SIO KWAMBA alikuwa kwenye msafara wa Mwenge kama inavyoenezwa.

Ally aliyezaliwa mkoani Shinyanga Machi 1, mwaka 1984 katika familia ya watoto sita, kabla ya umauti wake inafahamika alikuwa anaishi Yombo Vituka, Dar es Salaam.

Lakini tangu baada ya uchaguzi Mkuu Novemba 2015, Ally Yanga ameadimika viwanja vya soka kutokana na kujikita zaidi kwenye shughuli za Chama cha Mapinduzi CCM.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI