NCHI ya Marekani huenda ikawa imepata pigo kubwa kutokana na kuripotiwa kuwa Makomandoo wake Saba,wamepotea baharini.
Makomando
saba wa kikosi cha maji cha jeshi la Marekani wameripotiwa kupotea
baada ya meli yao kugongana na meli ya wafanyabiashara karibu na pwani
ya Japan.
Kamanda wa meli hiyo maalum za kuwaharibu maadui inayofahamika kama USS
Fitzgerald aka Destroyer, aliokolewa na kukimbizwa hospitalini kwa chopa
(helicopter).
Meli hiyo iligongana na meli ya wafanyabiashara iliyokuwa na makontena
umbali wa kilometa 104 Kusini-Magharibi mwa Yokosuka. Picha zilizopigwa
kutoka juu zilionesha uharibifu mkubwa kwa meli hiyo kutokana na tukio
hilo lililotokea majira ya saa nane na nusu usiku wa kuamkia leo, kwa
muda wa Japan.
Kwa mujibu wa BBC kamanda mwingine wa meli hiyo, Cdr Bryce Benson
ameokolewa na anaendelea kupata matibabu hospitalini lakini hali yake
imezidi kuimarika baada ya kuhamishiwa katika hospitali ya jeshi la
Marekani iliyoko Yokosuka.
Hadi kufikia majira ya asubuhi, taarifa zilizotolewa na maafisa wa jeshi
la maji la Marekani zimeeleza kuwa ingawa ‘Destroyer’ ilikuwa katika
hatari ya kuzama, maeneo yote ya kuingilia maji ndani ya meli hiyo
tayari yameshadhibitiwa kitaalam.