Saturday, June 10, 2017

KAMATI YA PILI YA KUCHUNGUZA MCHANGA WA MADINI ( MAKINIKIA ) KUKABIDHI RIPOTI YAKE JUMATATU

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO



RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,John Magufuli, Jumatatu anatarajia kukabidhiwa  taarifa ya kamati ya pili ya wachumi na
wanasheria iliyofanya uchunguzi wa mchanga wa dhahabu ( Makinikia ) uliokuwa katika makontena 227,yanayomilikiwa na Kampuni ya Madini ya Acacia.

Mchanga huo wa madini uliokuwa kwenye makontena,ulizuiliwa kusafirishwa nje ya nchi kama ilivyokuwa ada yake,na kuundiwa tume mbili,ambapo Kamati ya awali iliishakabidhi Ripoti yake,na kubakiwa na ile ya pili,ambayo nayo tayari imeshakamilisha majukumu yake,na kuwa tayari kuikabidhi kwa Rais Magufuli.

Taarifa iliyotolewa leo (Jumamosi) na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imesema tukio hilo litarushwa hewani moja kwa moja kupitia redio, televisheni, mitandao ya kijamii na tovuti rasmi ya Ikulu ambayo ni www.ikulu.go.tz kuanzia saa 3:30 asubuhi.

Ikulu imewakaribisha wananchi kufuatilia matangazo hayo kupitia vyombo hivyo au simu za mkononi kwa kutembelea tovuti hiyo.

Mei 24, Rais Magufuli alipokea ripoti ya kamati ya kwanza yenye wajumbe wanane iliyochunguza aina na viwango vya madini yaliyomo kwenye mchanga wa madini uliomo ndani ya makontena yaliyozuiliwa na Serikali kusafirishwa nje ya nchi.

Kamati hiyo aliiteua Machi 29, mwaka huu ikiwa na wajumbe ambao ni wana taaluma katika fani za jiolojia, kemia, uhandisi kemikali na uhandisi uchenjuaji madini.

Baada ya kuipokea ripoti hiyo, Rais Magufuli alitengua uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.

Rais Magufuli pia aliivunja Bodi ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) na kumsimamisha kazi mkurugenzi mtendaji wake.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI