Sunday, June 11, 2017

IGP SIRRO AWATOA HOFU WATANZANIA JUU YA MAUAJI YANAYOTOKEA PWANI

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO



MKUU wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro, amewatoa hofu Watanzania juu ya


kinachoendelea Mkoani Pwani kuhusiana na mauaji,kwa kudai wapo mbioni kukomesha vitendo hivyo.

Watanzania wametakiwa katika kipindi hiki kuwa na imani na Jeshi hilo huku wakiwa wavumilivu kwa kuwa Polisi wanafanya uchunguzi wa kina kuhusu mauaji yanayoendelea mkoani Pwani.

Sirro alisema hayo jana (Jumamosi) katika ziara yake ya kwanza mkoani Morogoro tangu ateuliwe kuwa IGP na kusisitiza kuwa polisi wanafanya kazi usiku kucha kudumisha hali ya usalama.

“Hatulali, tunafanya kazi kwa juhudi kubwa, lakini ni lazima wananchi watupe ushirikiano na nyinyi waandishi wa habari pia mnatakiwa mwandike kwa hekima bila uchochezi,” amesema. 


Sirro amesema amefanya ziara hiyo Morogoro na katika maeneo mengine nchini ili kuzungumza na polisi namna ya kusimamia ulinzi na usalama katika maeneo yao

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI