SERIKALI sasa
kuwatambua wafanyabiashara wadogo wadogo wasio rasmi wakiwamo mama lishe na
baba lishe,machinga kwa kuahidi kuwapa
vitambulisho maalumu vitavyosaidia
kuwatambua rasmi.
Aidha haitaruhusu usafirishaji wa madini moja kwa
moja kutoka mgodini na kupelekwa nje ya nchi.Huku ikitangaza kufuta rasmi kwa
ada ya mwaka ya leseni ya magari.
Hayo yalielezwa
jana Alhamisi na Waziri wa Fedha na Mipango, Phillip Mpango wakati akiwasilisha
hotuba ya bajeti kwa mwaka 2017/18. Ambapo alibainisha kwamba
vitambulisho hivyo vitawasaidia kutengewa maeneo maalumu ya kufanyia biashara.
Akiwasilisha
mapendekezo ya bajeti kuu kwa mwaka wa fedha 2017/18,ambayo ilikuwa
ikishangiliwa kwa vifijo na nderemo na wengi wa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania,Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mpango alisema hatua hiyo
inalenga kuwasaidia wafanyabiashara hao ili kukuza mitaji yao.
Sambamba na
hilo Serikali imetangaza kufuta ushuru wa huduma kwenye nyumba za kulala
wageni.
Pamoja na
ushuru huo, pia Serikali imefuta ushuru wa mabango yanayoelekeza mahali zinapopatikana
huduma za kijamii kama vile shule na hospitali.
Kadhalika
alisema Serikali kwa dhati imeamua kufuta tozo la malipo ya leseni wa
gari,ambao ulikuwa ukilipwa kila mwaka.
Alisema uamuzi huo umechukuliwa ili ada hiyo ilipwe
mara moja pale gari linaposajiliwa na baada ya hapo iendelee kulipwa katika
ushuru wa bidhaa katika mafuta ya petroli na dizeli.
Pamoja na
hayo, Waziri Mpango ameshusha ushuru kwa mvinyo unaotengenezwa kwa
zabibu zinazozalishwa ndani kutoka Shilingi 2O2 kwa lita hadi Shilingi
200 kwa lita.
Hata hivyo
alisema ushuru wa bia zinazotengenezwa kwa nafaka za ndani umepanda kutoka Shilingi
429 hadi 450 kwa lita.
Wakati
huo, ushuru wa bia zisizo na kilevi na vinywaji vya kuongeza nguvu kutoka
Shilingi 534 hadi Shilingi 564 kwa lita.
Aidha
alisema Serikali imesitisha utaratibu uliokuwa ukifanywa na Wawekezaji katika
shughuli za madini nchini za kusafirisha bidhaa hiyo moja kwa moja kutoka
viwanja vyao vya Migodi,badala yake kutakuwa na viwanja maalumu vya kimataifa
katika bandari, migodini na madini hayo yatathibitishwa na kupewa kibali kabla
ya kusafirishwa nje.
“Kibali
hicho kitatozwa ada ya asilimia moja ya thamani ya madini hayo,” amesema.
Amesema
Serikali itatangaza rasmi tarehe rasmi ya kuanza kwa ada hiyo.