MAPEMA
Januari,Mwaka huu,bweni katika Shule ya Sekondari Mwendakulima,liliteketea kwa
moto na kusababisha
wanafunzi kuanza kuishi katika mazingira ya tabu.
Katika
ajali hiyo ya moto,ambayo haikusababisha madhara ya kifo ama jeraha kwa
mwanafunzi yeyote,imekuwa sababu ya wanafunzi hao kupata chakula wakiwa nje
kufuatia bwalo lililokuwa la chakula,kutumika kwa ajili ya kulala wanafunzi.
Wanafunzi
katika shule hiyo yenye Kidato cha kwanza hadi cha sita,wamejikuta wakilazimika
kuketi katika vivuli vya miti,muda unapowadia wa chakula,kitendo kinachodaiwa
kupunguza ari ya kusoma kwa wanafunzi hao.
Hali
hiyo ilielezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Kahama,Anderson
Msumba,katika uzinduzi wa ujenzi wa jengo jipya la bweni ulioambatana na msaada
wa vitabu 1312 vya masomo ya Sayansi kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi
cha nne vyenye thamani ya Shilingi Milioni 24,vilivyotolewa na Mgodi wa
Buzwagi.
Msumba
alibainisha tangu kuungua kwa bweni hilo,Januari mwaka huu,kumelazimisha vijana
wanaosoma katika shule hiyo,kupata chakula wakiwa wameketi chini ya
miti,kufuatia uongozi wa shule hiyo kuligeuza bwalo kuwa chumba cha
malazi,kitendo ambacho wana imani kinashusha morari ya vijana kusoma.
Alisema
kwamba kabla ya tukio la moto,waliwasilisha maombi katika Mgodi wa Buzwagi
usaidie kujenga bweni lingine kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi kufuatia
shule hiyo kuwa na kidato cha kwanza hadi cha sita,ombi ambalo lilikubaliwa na
uongozi wa Mgodi.
“..lakini
kabla ombi hilo kutekelezeka,bweni lililopo likaungua na kusababisha wanafunzi
waishi katika mazingira magumu,huku mgodi ukiwa kimya katika kutekeleza ahadi
yake,nilikata tamaa,sasa nafarijika kuona umedhamiria kukamilisha ahadi yake.”Alisema
Msumba.
Kwa
upande wake,Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi unaomilikiwa na Kampuni ya
ACACIA,Stewart Hamilton,alisema watahakikisha ahadi zote walizoahidi
zinatekelezeka,kuanzia zile za sekta ya elimu hadi sekta ya afya.
Alifafanua
katika mradi waliahidi wa ujenzi wa bweni,wamepanga kutumia Shilingi Milioni
214,na kwmba jengo hilo litakapo kamilika litasaidia kurejesha hali ya kawaida
shuleni hapo kwa matumizi ya bwalo kutumika kama ilivyokusudiwa.
Nae
Makamu Mkuu wa Shule hiyo,Sonda Kenda,alisema msaada wa vitabu waliopokea
sambamba na kuanza kwa mradi wa ujenzi wa jengo la Bweni,wameutarajia kwa
kipindi kirefu na utajenga hamasa kubwa kwa wanafunzi kuhakikisha wanafanya
vyema katika masomo yao kwakuwa yatakuwa yamewajengea mazingira mazurin ya
kupata elimu.