IDARA ya Magereza Nchini ni moja ya Taasisi muhimu nchini,kutokana na kuwajibika kulinda katika maisha ya kila siku;Watuhumiwa na Wafungwa,wanaojumuika nao
katika maisha ya kila siku kwa mujibu wa sheria,huku askari wake wakikabiliwa na changamoto ya kuishi katika Mazingira Duni.
katika maisha ya kila siku kwa mujibu wa sheria,huku askari wake wakikabiliwa na changamoto ya kuishi katika Mazingira Duni.
Changamoto hizo zimeuvuta Mgodi
wa Dhahabu wa Buzwagi,unaomilikiwa na Kampuni ya Uchimbaji madini ya ACACIA,kutumia
Jumla ya Shilingi Milioni 12.8,kujaribu kupunguza changamoto ya makazi inayoikabili
Idara ya Magereza wilayani Kahama,ambayo askari wake wanaishi familia nne
katika nyumba moja.
Kwa
mujibu wa Mkuu wa Gereza wilaya ya Kahama,SSP Isani Mjimbi,alisema Idara hiyo
ina changamoto kubwa ya makazi kutokana na kuwa na nyumba kumi na sita huku
baadhi yake zikiwa duni,hali iliyowafanya kuomba msaada katika Mgodi huo.
Katika
makabidhiano ya vifaa hivyo,Meneja wa Mgodi wa Dhahabu Stewart Hamilton,alisema
wametoa vifaa hivyo ikiwa ni jukumu lao la kusaidia huduma za jamii katika
wilaya ya Kahama,baada ya kuombwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya
wilaya,kusaidia idara hiyo.
Alisema
msaada huo ni katika jitihada za kuunga mkono,Idara ya Magereza wilaya ya
Kahama za kujenga Maboma kwa lengo la kupunguza upungufu wa nyumba za makazi kwa askari ambao wamekuwa
wakiishi katika makazi duni,huku wakilazimika kuchangia nyumba moja zaidi ya
familia nne.
Hamilton
alivitaja vifaa vilivyotolewa kwa ajili ya kukamilisha boma moja lenye uwezo wa
kubeba familia nne,ni mifuko ya saruji 51,bati 96,misumari kilo 29,milango
12,trip 10 za michanga,Trip nne za kokoto na trip sita za mawe.
Akizungumza
wakati wa kupokea Misaada hiyo,Mkuu wa Gereza la Kahama, SSP Isani Mjimbi,alisema
idara hiyo yenye jumla ya askari 80 inakabiliwa na upungufu wa nyumba zaidi ya kumi,huku zilizopo 16 zikidaiwa kuwa ni
chakavu kutokana na kujengwa mwaka 1957.
SSP
Mjimbi alisema kutokana na nyumba zilizopo kuwa pungufu na nyingine zikiwa duni
hali imewafanya askari kuishi katika mazingira magumu yanayowalazimisha askari kugawana chumba
kimoja kimoja kwa kila familia.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kahama,Fadhili Nkurlu aliziomba taasisi na
makampuni mbalimbali wilayani Kahama,kujitokeza kutatua changamoto zinayoikabili
Idara ya Magereza,kutokana na umuhimu wake katika Jamii.
Nkurlu
alisema Idara hiyo pamoja na kukabiliwa na matatizo mbalimbali imekuwa
ikionesha jitihada za kufyatua tofari na kujenga maboma,hivyo jamii sambamba
na mashirika pia kampuni zinapaswa
kuunga mkono jitihada zinazofanywa na idara hiyo katika kujinasua na makazi
duni.