Tuesday, May 2, 2017

RAIS MAGUFULI ATANGAZA KIAMA CHA WALIODANGANYA UMRI SERIKALINI

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO



 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk. John Pombe Joseph Magufuli, ametangaza kiama
cha baadhi ya wafanyakazi waliofanya hila ya kupunguza umri ili wadumu kipindi kirefu katika ajira.
Amesema baada ya vyeti feki na vya kughushi kuna ombwe la baadhi watumishi wamebadili umri wao ili waendelee kuwepo kwenye ajira serikalini,na kudai wafanyakazi waliotenda jambo hilo watachunguzwa na kuwachukuliwa hatua kali.

Akizungumza jana kwenye sherehe ya sikukuu ya wafanyakazi dunia zilizofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanajaro, alisema wapo wafanyakazi ambao wamebadilisha umri wao na wanaendelea kuwepo kwenye ajira licha ya kwamba wamezeeka na walistahili kustaafu.

Anasema,“Wapo watumishi ambao wamebadilishi umri wao wa kuishi wamebadilisha miaka yao, unakuta ni mzee kabisa lakini yeye hastaafu tu huyo naye hana utofauti sana na mfanyakazi hewa, kwa sababu ameshamaliza muda wake hataki kutoka kazini awaachie wengine nao wafanye kazi anaendelea kukaa pale kubadilisha miaka,” 

“Mimi hapa nilipo nilikuwa nimebakiza miaka miwili tu kustaafu lakini hebu kaangalieni kwenye maofisi yenu wapo watu ambao ni wazee kuliko mimi bado wanafanya kazi na wanasema ndio wakati umefika, hawa nao dawa yao tunaichunguza,”Anasema. 

Aidha Rais Magufuli alisema serikali yake imefaulu kwa asilimia Tisini na nane katika zoezi la kuondoa wafanyakazi hewa,na kudai pamoja na hatua hiyo kufanikiwa kwa asilimia hizo,jambo linalotia faraja lakini bado halijaisha. 
Aliongeza kuwa katika fedha tu za watumishi hewa, ukichukulia tu mshahara serikali ilikuwa inapoteza Sh. bilioni 19.8 kwa mwezi na kwa mwaka ni zaidia Sh. Bilioni 230.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI