Friday, April 28, 2017

SERIKALI YAFUTA AJIRA 9932 KWA KUBAINIKA KUWA NA VYETI FEKI

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk. John Pombe Magufuli, ameiagiza kufutwa kazi kwa Watumishi
9,932 waliobainika kutumia vyeti vya kughushi vilivyokuwa na msaada mkubwa wa kupata ajira.
Rais Dkt.Magufuli ametoa agizo hilo kwa Wizara ya Fedha kufuta mara moja ajira za  watumishi hao wa umma, waliobainika kupata ajira  kwa kughushi vyeti, kwenye orodha ya malipo ya watumishi wa umma.

Akiongea   mara baada ya kupokea ripoti ya uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma mjini Dodoma, Rais Magufuli pia amewataka watumishi hao kuondoka wenyewe na iwapo watakaidi wakamatwe na vyombo vya dola na kushtakiwa.

Rais Dk. Magufuli pia ameziagiza mamlaka husika kujumuisha nafasi 9,932 za ajira ambazo zimeachwa wazi na watumishi wa umma walioghushi vyeti, kwenye ajira mpya zaidi ya elfu 52 za serikali ili ziweze kuchukuliwa na watu wenye sifa na uwezo wa kumudu nyadhifa zilizoachwa.

Akizungumza wakati akiwasilisha ripoti hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki, amesema, kwa Mujibu  wa Kanuni na Sheria za nchi zinabainisha wazi kuwa mtu atakaebainika kughushi vyeti au kutoa taarifa za uongo adhabu yake ni pamoja na kifungo cha Jela.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI