RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,John Pombe Joseph Magufuli,amejinasibu kutenda haki mara atapopata
ripoti ya watumishi wa
Serikali,waliogushi vyeti.
Kuna madai ya wafanyakazi wa
Serikali zaidi ya elfu tisa kutumia vyeti vya kufoji,ambapo sasa Rais Magufuli,
amefunguka kwa kusema sasa anasubiri ripoti ya wahusika hao ili aitendee kazi.
Rais Magufuli amesema hayo, wakati
akizindua majengo ya Hostel za Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM),kwa kudai kumekuwa
na changamoto kubwa katika kila sekta hivyo sasa anasubiri hiyo ripoti ili
aweze kuifanyika kazi na kutenda haki katika jambo hilo.
Anasema;"Naisubiri
ripoti ya wafanyakazi wa Serikali zaidi ya elfu tisa ambao wana vyeti vya
kufoji ili niifanyie kazi."
Mbali na hilo Rais Magufuli ameitaka
Taasisi ya TCU kuacha kuwapangia wanafunzi vyuo bali wanafunzi wanapaswa kuwa
huru kuchagua aina ya vyuo ambavyo wao wanataka kwenda kusoma.
Amefafanua kwa kusema kufanya hivyo
itatoa nafasi kila chuo kuwa na wanafunzi wa kutosha huku wanafunzi pia
wakienda kusoma sehemu ambazo wao wanahitaji kwenda kusoma na si kuwapangia.
"Mtu
amefaulu ana sifa zake anataka kuja kusoma Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam afaidi
mabweni ya Magufuli analazimishwa kupelekwa kwenye ka chuo ambako wala hakana
jina hata ukitafuta kwenye mtandao hakaonekani, akasome pale wakati hawana hata
mabweni na saa zingine hata walimu hawana, tunawatesa watoto hawa,”
“… na saa
zingine wakuu wa vyuo vile wamekuwa na tabia ya kwenda kwenye uongozi wa TCU
ingawa sina ushahidi wapangiwe idadi wa wanafunzi wanaowataka kwenye vyuo
hivyo,”
“….sifahamu
wanapangiwa kwa rushwa,lakini wapo pia kuna ushahidi na baadhi ya viongozi wa
vyuo fulani fulani waliofunga safari kwenda TCU kwa ajili ya kuomba wapangiwe
wanafunzi au kutoa shukrani, au hata kwenda kuwasalimu tu" alisema Rais Magufuli.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI