BARAZA
la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Kahama mkoani Shinyanga,wameamuru
kukamilishwa mara moja kwa ujenzi uliotumia miaka 11 katika Shule ya Sekondari
Kitwana,iliyoko Kata ya Busoka,ili kunusuru wanafunzi
kutembea umbali wa kilometa 15,kufuata masomo.
kutembea umbali wa kilometa 15,kufuata masomo.
Maazimio
ya Baraza hilo yalifikiwa juzi,baada ya Diwani wa Kata ya Busoka,Julius Malale,kuwasilisha
malalamiko ya wananchi wa Kijiji cha Kitwana,wanaohitaji kurejeshewa
maeneo yao waliyoyatoa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari Kitwana,ambao
umeshindikana kukamilika.
Katika
malalamiko hayo,Wananchi hao wamedai hawaoni faida ya kuyatoa maeneo hayo na
kuhitaji kurejeshewa,kutokana na kutokamilika ujenzi wake kwa miaka 11,huku Shule
nyingine zilizoanza ujenzi wake hivi karibuni zikikamilika,ilhali vijana wao
wakiendelea kuteseka kutembea umbali zaidi ya kilometa 15 kufuata shule katika
kata jirani.
“…kuna
shule zilizoanza ujenzi na Kitwana zimekamilika na kuanza kutumika,zingine
ujenzi wake umeanza hivi karibuni nazo zinafanya kazi,sasa wana kijiji hao waliotoa
maeneo hayo wanadai leo ni miaka 11,imeshindikana kumaliza ujenzi huo wa
sekondari,warejeshewe maeneo yao,kwani hayana tija tena kwa elimu,” alisema
Malale.
Kwa
upande wake Diwani wa Kata ya Kahama mjini,Hamidu Kapama,aliliambia baraza hilo
kutokamilika ujenzi kwa sekondari hiyo,ni uzembe uliosababishwa na halmashauri
kupitia afisa elimu sekondari kwakuwa serikali imekuwa ikiongea bila
utekelezaji suala ambalo linawakatisha tamaa wananchi.
Akijibu
malalamiko hayo Ofisa elimu sekondari,Anastazia Manumbu, aliliambia baraza hilo
kuwa bado halmashauri inaendelea na mchakato wa ukamilishaji wa sekondari hiyo
kwa kubainisha kwamba kwa kipindi hiki wanaendelea na ujenzi wa vyoo na nyumba
ya mwalimu.
Hata
hivyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Kahama,Abel Shija,alihitimisha
mjadala na kuungwa mkono na madiwani wote kwa kumtaka Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri hiyo,Kapami,kuhakikisha Sekondari hiyo,inakamilika mapema
iwezekanavyo, kwa kutumia mafungu ya dharura iwapo kama haikupangiwa bajeti.