SIR Jayantilal Keshavji 'Andy' Chande,aliyekuwa kiongozi wa Jumuiya ya Freemason Tanzania na Afrika Mashariki, amefariki Dunia.
Sir Andy ambaye amedumu Uanachama wa Freemasons kwa takribani miongo 6 tangu ajiunge,alizaliwa Mombasa, Kenya Mei 7 ,1928 japokuwa wazazi wake walikuwa wakiishi Bukene Mjini, Mkoani Tabora (Tanzania).
Hadi umauti unamfika sehemu kubwa ya maisha yake yalikuwa nchini Tanzania.
SIR ANDY CHANDE NA FREEMASONS
Freemasons
wamekuwa wakitajwa kwenye kila aina ya minong’ono. Tumeona matangazo
yakialika watu kujiunga nao kama wanataka kupata utajiri na kuwa watu
wenye nguvu. Lakini bado Freemason, imebaki kuwa kitendawili miongoni
mwa Watanzania wengi.
SIR Andy Chande kushoto akiwa na wana Freemasons wenzake. |
Katika uhai wake,Sir Andy Chande,ambaye ni Mtanzania maarufu, alifungua kinywa chake na
kueleza namna alivyojiunga na Freemasons, kundi lililo kongwe duniani.
Tayari
watu mbalimbali watu wenye hamu ya kupata utajiri wamekuwa wakitoa
ushuhuda kuhusu kundi hilo na kusikika kwenye vyombo vya habari, hasa
baada ya kifo cha mwingizaji nyota, Stephen Kanumba, mwaka 2012.
Siyo
hivyo tu, bali kumeibuka pia matangazo yenye namba za simu
yanayoshuhudiwa kwenye nguzo za simu mitaani hadi vichochoroni
yakiwataka watu wanaotaka kujiunga na Freemason kupiga simu ili wapewe
utaratibu wa namna ya kujiunga kwenye ‘kisima hicho cha mafanikio’.
Baadhi
ya watu tayari wameshanaswa na mtego huo, huku wengine wakiendelea
kujaribu bahati yao kujipatia utajiri kwa njia ya ‘nguvu za giza’.
AKIWA na Rais wa Awamu ya Kwanza,Tanzania;Mwalimu J.K.Nyerere. |
Hata
hivyo Jayantilal Keshavji Chande, maarufu zaidi nchini kwa jina Sir
Andy Chande, aliyejiunga na Freemason Oktoba 25, 1954 baada ya kupita
kwenye usaili mzito, anaeleza namna alivyoibuka kutoka familia ya
kawaida hadi kuwa kiongozi wa Freemason Afrika Mashariki.
Sir
Andy Chande, ambaye amekuwa mwanachama wa kundi hili kwa karibu miongo
sita sasa, anaeleza namna alivyosajiliwa na kufikia hatua ya juu ndani
ya kundi hilo.
Chande
alizaliwa Mombasa Kenya, Mei 7, 1928, ingawa wazazi wake walikuwa
wakiishi Bukene mjini, mkoani Tabora, magharibi mwa Tanzania.
AKIWA na Rais wa Awamu ya Pili ya Tanzania,Alhaj Ali Hassan Mwinyi. |
Katika
kufafanua utaratibu mzima wa Freemason, Chande ameandika kitabu
alichokiita; ‘A night in Africa-a journey from Bukene’ (Usiku wa
Afrika-Safari kutoka Bukene), pengine akitaka kuweka sawa dhana na
kuondoa tofauti ili misingi inayoendesha Freemason ifahamike.
Imani
ya kimaadili na thamani ya kundi hilo ilianza wakati wa mazungumzo yake
na Messrs Campbell Ritchie na McLean mwanzoni mwa miaka ya 1950.
“Katika
kipindi kile nilianza kutambua kuwa Freemason ipo katika msingi wake.
Ni sayansi ya maisha ambayo malengo yake ni kumbadilisha mtu kiimani na
kumfanya awe anavyopaswa kuwa. Ni mabadiliko ya mtu binafsi,” Sir Andy
Chande ameandika katika kitabu chake chenye kurasa 207.
Anasema
kuwa malengo ya Freemason yamefunikwa na mafumbo, ambayo pengine ndiyo
yanayoeleza utamaduni uliojificha katika utendaji kazi wake.
HAPA akiwa na Rais wa Awamu tatu,Tanzania;Benjamin Mkapa. |
Chande
anabainisha kuwa kanuni kubwa tatu za Freemason ziliandikwa kwenye
kitabu kimoja nchini Canada, kilichochapishwa na Kampuni ya Penumbra
Press.
Anaandika:
“Kwa hiyo, ukiwa kwenye ngazi ya kwanza (first degree), kanuni
inayoongoza, inamtaka mtu awe mkweli na mwenye maadili ambayo hasa
Freemason inalenga kuyaweka kwenye akili, ili mwanachama awe mzuri.
Ngazi
ya pili ya utaratibu inatilia mkazo kwenye vipaji na akili kupitia
sanaa na sayansi, ili kutoa mchango mzuri iwezekanavyo kwenye maisha.”
Anafafanua
kuwa ngazi ya tatu inampa mtu nafasi ya kutafakari uwepo wake kwa kina
na kwamba kanuni zote tatu zinafahamika kama upendo wa kindugu, kujiweka
huru na ukweli.
“Kwa
njia hizi inamaanisha, unafundishwa namna ya kuyafurahia maisha kwa
kiwango chake cha juu. Kwa kufuata hizo kanuni tatu za upendo wa
kindugu, kujiweka huru na ukweli, wakati huohuo ukijitambua na kuanza
kujiandaa na kutokwepeka kwa kifo,” anaandika Chande.
Anaongeza
kuwa, wakati kanuni hizo tatu zinapoondolewa kwenye alama ya sanaa
inayofunika imani ya Freemason, ambazo zilimpa udadisi wa kupata taarifa
kuhusu utaratibu huo wa kale.
Sir Andy Chande ni Kiongozi wa Freemason Afrika Mashariki.
Kanuni za Freemason zinafundisha nini?
Katika
ratiba ya Freemason, anaandika Chande akieleza kuwa, kanuni ya upendo
wa kindugu inawafundisha ndugu wote kuwachukulia wanadamu wote kama
familia moja iliyoumbwa na nafsi moja kuu.
“Kujiweka
huru, vilevile, inaleta ujumbe nilioupata kutoka kwa baba yangu,
aliyesema ni kuwekwa huru kwa mtu mwenye msongo. Kama ni kuwekwa huru
kutoka kwenye umaskini, matatizo au akili isiyo na furaha,” anaandika
Chande katika kitabu hicho.
Anafafanua kuwa ngazi ya tatu ambayo ni ukweli na pengine ndiyo muhimu zaidi ni mchango wa kimungu kwa mwanachama wa Freemason.
Anabainisha
kuwa kipindi hicho ndicho kinachoheshimika kama njia ya matazamio na
marekebisho na kama inawezekana, kurudiwa kwa kanuni hizo kama msingi wa
kuelekea kanuni kuu nne alizozitaja kuwa ni; udhibiti binafsi, nguvu,
umakini na haki.
ALIPOKUTANA na Rais wa Awamu ya Nne,Tanzania;Jakaya M.Kikwete. |
Chande
anaeleza kuwa Freemason siyo kifaa cha dini, pia siyo mpinzani wa dini,
lakini inakaribisha watu wote bila kujali dini zao na haijaribu
kubadilisha imani zao au kushawishi kuabudu kwao.
“Inajaribu tu kuwafanya watu kuwa wema,” anaandika Sir Chande akifafanua:
“Hii
ndiyo dunia niliyoingizwa mwaka 1954, imekuwa na mchango mkubwa katika
maisha yangu tangu wakati huo…: Roho yangu, akili yangu na nafsi yangu,
vimetajirishwa na kushiriki kwangu Freemason.
Akiwa na Diamond Platnumz