WAMILIKI wa Nyumba za Kulala Wageni na Hoteli mkoani
Iringa (Iloha),wamekataa kulipaushuru wa hoteli hadi watakapoonana na uongozi wa
mkoa.
Akizungumza katika mkutano huo,Katibu Mkuu wa Iloha,Adam Lameck alisema watalazimika kusitisha utoaji huduma kutokana na mlolongo wa kodi zinazowakabili.
“Endapo hatutasikilizwa, tunafunga biashara zetu mpaka hapo tutakapopata muafaka,” alisema.
Mmiliki
wa Nyumba ya Wageni, Zakaria Mdeka alisema tangu mwaka 2008 kodi hiyo
ilifutwa lakini wao waliendelea kulipa kwa asilimia 10 bila kuzingatia
mmiliki anaingiza shilingi ngapi.
Wafanyabiashara
hao wamedai wamekuwa wakitozwa mlolongo mkubwa wa kodi zaidi ya 23
ambazo zote zinatakiwa kulipwa bila kuzingatia mmiliki anapata faida
kiasi gani.