VIONGOZI wa dini zote
nchini,wametakiwa kushirikiana pasipo kujali tofauti zao za kiimani ili nchi
iwe na amani na usalama.
Ushauri huo ulitolewa na
Mufti Mkuu wa Tanzania,Sheikh Abubakar Zuberi bin Ally,jana Jijini Dar Es
Salaam,wakati wa ufunguzi wa semina elekezi kwa viongozi wa Baraza Kuu la
Waislamu Tanzania(Bakwata).
Mufti Zuberi alisema
viongozi wa dini wanapaswa kushikamana pasipo kuangalia tofauti zao za kiimani
kwakutambua kuwa wana mchango mkubwa katika kuhakikisha usalama na amani
inadumu hapa nchini,na kusihi kuepuka kuibuka tofauti za kidini zitakazotishia
utulivu uliopo nchini.
“Nyumba ni moja,hakuna
sababu ya kugombea fito.Sisi ni waumini wa kiroho,ili waumini waweze kufaulu na
kupata pepo tuna jukumu la kuwaunganisha kuwa kitu kimoja,”alisema.
Pamoja na hilo,aliwahimiza
waumini hao kutafuta riziki halali.
Kwa upande Sheikh wa Mkoa
wa Dar Es Salaam,Alhad Mussa,alisema pindi viongozi wa pande zote za dini
wakishikamana kwa dhati amani na usalama utadumu hivyo kuwafanya wananchi
kutoka mataifa mengine kuwa kimbilio,hatua ambayo itasaidia kukuza uchumi wa
taifa.