Na Jackson Bahemu,
RAIS wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli, amepunguza kodi ya mshahara kwa watumishi
(PAYE) toka asilimia 11 mpaka asilimia 9 huku akiwataka waajiri wote nchini kuhakikisha
wanawapa mikataba ya ajira wafanyakazi wao .
Rais ameongeza kuwa waajiri waakikishe makato ya mapato yao yanafikishwa katika mifuko ya kijamii bila kukosa na kuwataka watumishi kumvumilia kwani hataweza kuwaongeza mshahara bali anapambana kuinua uchumi na kuziba mianya ya rushwa na ufisadi.
Aidha ameelezea juu ya zoezi linaloendelea nchi nzima la watumishi "misukule"kuwa mpaka jana ni watumishi hewa 10,295 huku watumishi 8,373 wanatoka Tamisemi na 1,922 wakiwa ni watumishi toka serikali kuu.
Akifafanua hasara iliyosababishwa na watumishi
misukule wameigharimu serikali bilioni 11.6 kwa mwezi sawa na bilion 139 kwa
mwaka mzima.
Akihitimisha hotuba yake Rais Magufuli amewataka wafanyakazi wote kuwa wachapakazi na kuwawaadifu katika majukumu yao pia kuwa wazalendo kwa nchi yao.