VIGOGO
wa Chama cha Wananchi CUF,wanashikiliwa na Jeshi
la Polisi Zanzibar kwa tuhuma za kupanga na kuhusika katika
uratibu,utengenezaji na ulipuaji wa mabomu kisiwani Zanzibar.
Akitoa
taarifa kwa vyombo vya habari Naibu Mkurugenzi wa upelelezi na Makosa
ya Jinai Zanzibar Kamishina Msaidizi wa polisi Salum Msangi amesema
watuhumiwa hao wamekamatwa baada ya upelelezi wa kisayansi wa Polisi
huku akisema wengine ni viongozi wa juu wa CUF na wasomi na wataalamu wa
Chuo Kikuu cha Zanzibar ambapo lengo lao likuwa ni kulipua makazi ya
Makamu Wapili na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar .
Watuhumiwa
waliokamatwa ni Omar Bakari Nassor,Hassan Omar Issa Mwenyekiti wa CUF
wilaya ya Magharibi Salehe Mohamed Saleh Katibu wa CUF Magharibi na
Suleiman Mohmaed Bakari Katibu wa CUF Mfenesini.
Mkuu
huyo wa upelelezi amesisitiza na kutoa onyo kuwa Jeshi la Polisi
halitasita na linaendelea na kazi ya kuweka ulinzi kwa wananchi na
yeyote au kikundi kitakachojaribu kuleta fujo polisi imejiandaa
kikamilifu.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI